Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 9 February 2019

WAFANYAKAZI WA COCA-COLA KWANZA NA WADAU WA MAZINGIRA WAFANYA USAFI KATIKA FUKWE ZA COCO

Wafanyakazi wa Coca Cola Kwanza na Wananchi wengine waliojitokeza wakifanya mazoezi ya kuchangamsha mwili (Aerobics) mapema asubuhi ya leo kabla ya kuanza zoezi la usafi katika fukwe za Coco.
Msanii na Balozi wa Coca Cola Kwanza Mrisho Mpoto (Mjomba) akitoa burudani na ujumbe kwa jamii iliyokusanyika hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Daniel Chongolo akiipongeza kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kampeni yao ya "Mchanga Pekee". Pia ameipongeza kampuni ya EcoAct Tanzania kwa ubunifu wa kutengeneza vibao vya alama za barabarani kutumia Plastic tofauti na chuma ambazo watu huzing'oa na kwenda kuuza vyuma chakavu.
Tania Hamilton, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio akishiriki kusafisha fukwe ya Coco.
Mrisho Mpoto (kushoto) Basil Gadzios, Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola Kwanza Tanzania (Katikati) na Tania Hamilton (Kulia) wakijadilia jambo.
Mtoto aliyejitokeza na kuimba wimbo wa Mrisho Mpoto mahususi kwa kutunza Mazingira.
IFAHAMU KAMPENI YA MCHANGA PEKEE YA COCA-COLA KWANZA
Mchanga Pekee
Mchanga pekee ni Kampeni iliyobuniwa, kuasisiwa na kusimamiwa na Kampuni ya Coca-Cola kwanza Kampuni Tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa yenye malengo na madhumuni ya kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.

Chimbuko la Kampeni (Mchanga Pekee)
Shirika la International Council of Beverages Associations (ICBA) mwishoni mwa mwaka 2018 lilitoa ripoti inaoonyesha uchafuzi wa fukwe umefikia wastani wa vipande vya plastiki 13,000 kwa km2 za fukwe za baharini na utafiti wa karibuni umebaini kuwa kuna Tani million 150 za plastiki kwenye fukwe zetu duniani mpaka leo. Kupitia tafiti hizi na nyingine zilizopo Kampuni ya Coca-Cola Kwanza imeamua kuja na Kampeni yenye malengo ya kuikumbusha na kuishirikisha jamii juu ya Utunzaji wa mazingira kwa ukusanyaji wa taka (plastiki), uhifadhi wake na Ubadilishaji wa matumizi wa plastiki (recycling) kwa manufaa bora ya jamii na mazingira kwa ujumla.

Mchanga Pekee ni nini?
Ni kampeni ya mazingira yenye malengo ya usafishaji wa fukwe zetu na kuziweka katika mandhari salama,endelevu na zenya kuvutia yaani kuubakiza mchanga peke yake kwenye fukwe kwa kuondoa vitu visivyostahili kuwepo (uchafu-plastiki) na pia kampeni itajikita katika ukusanyaji wa chupa za plastiki katika mazingira yetu kuwezesha mazingira kuwa salama na yenye kuweza kuhifadhi ekolojia ya mazingira iliopo.

Usafishaji fukwe.
Kama lengo moja wapo wa kampeni ya Mchanga pekee kampuni ya Coca-Cola Kwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) ya kufanya usafi wa fukwe, na fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia kampeni yetu huku kampeni hii ikiwa na lengo la kufikia fukwe zote zilizopo nchini.
Coca Cola Kwanza itaajiri na kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapa vitendea kazi na posho ya kufanya usafishaji wa fukwe kwa kipindi chote (mwaka mzima) ambapo watakuwa na jukumu la msingi la kuhakikisha fukwe inakuwa katika hali ya usafi muda wote na kuhamasisha utalii wa fukwe kwa kuwezesha wale wanao tembelea fukwe kufurahia mandhari ya fukwe hizo katika mazingira yalio safi na salama.

Ukusanyaji taka (chupa za Plastiki) 10,000/Mwezi
Kama sehemu ya Kampeni hii ya Mchanga pekee Coca-Cola Kwanza pia imejikita kukusanya Chupa za plastiki 10,000 kwa kila mwezi kwa lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa ukusanyaji wa taka hizo (plastiki) na katika kampeni hii Coca-Cola Kwanza itazinunua chupa kutoka kwa jamii kupitia safari za utembeleaji wa jamii kwenye maeneo yao. Jamii itakusanya chupa na kampuni kuzinunua kwa bei iliopangwa kwa kipindi hicho, kampeni hii itaenda kwa kibwagizo chenye msemo wa “Trash 4 Cash”.

Faida na umuhimu wa Kampeni (Mchanga Pekee)
1.   Ufahamu na uelimishaji wa Uhifadhi na utunzaji endelevu wa mazingira yetu kwa ujumla.
2.   Kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga jamii bora yenye kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mzingingira na usimamizi endelevu wa mazingira.
3.   Ukuzaji wa sekta ya utalii wa fukwe kwa kuwezesha utunzaji wa fukwe wa muda wote na kufanikisha mvuto wa fukwe kama sehemu moja wapo ya kipato cha taifa kupitia sekta ya utalii.
4.   Uwezeshaji wa kiuchumu na kifursa (ajira) kwa vijana na wanawake kupitia mradi huu (mchanga pekee)
5.   Kupunguza ongezeko la chupa za plastiki katika jamii na kufundisha jamii njia bora za uhifadhi na ubadilishi bora wa matumizi ya chupa za plastiki.
6.   Ulinzi na uhifadhi wa ekolojia ya viumbe vya baharini na nchi kavu pia kuwezehsa jamii kuishi kwenye maeneo yaliyo huru na uchafu na maradhi yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Hitimisho
Kampuni ya Coca-Cola kwanza kama sehemu ya jamii na mdau mkubwa wa serikali na jamii katika uhifadhi wa mazingira imejipanga kuendeleza kampeni hii na kubuni kampeni nyingine tofauti tofauti zenye lengo la kuiwezesha jamii kuishi kwenye jamii ilio salama na endelevu ilikuwezesha shuguli za maendeleo kufanyika kwenye mazingira yaliyo bora na salama.

Imeandaliwa na
Idara ya mahusiano ya umma na mawasiliano

Coca-Cola Kwanza 

No comments:

Post a Comment