Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 16 November 2018

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ATAMBULISHWA BUNGENI, JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipomkaribisha Bungeni jijini Dodoma. Nsekela alimtembelea Spika Ndugai kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyemtemebelea Bungeni, jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Benki ya CRDB uliomtembelea Bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipungua wakati alipotambulishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, kwa Wabunge jijini Dodoma. 



Ujumbe wa Benki ya CRDB ukifatilia kikao cha Bunge, jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akibadilishana mawazo na baadhi ya Wabunge nje ya viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipokutana naye nje ya viwavja vya Bunge, jijini Dodoma.











No comments:

Post a Comment