Kampuni ya Simu za Mkononi Vodacom Tanzania imebainisha kuwa imejipanga kukabiliana na matatizo ya kiushindani sokoni ili kuhakikisha kampuni hiyo inaendelea kuwa kinara katika sekta hiyo ya mawasiliaano. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ali Mufuruki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wa wanahisa wa Vodacom Tanzania.
"Tumejipanga vizuri katika kukabiliana nayo, ya kwamba tunazo pesa za kutosha za kuwekeza na pia miundombuni mimpya na ya kisasa jambo ambalo linaufanya mtandao wa Vodacom kuwa bora na tumejipanga kiuhakika kuhakikisha kampuni inafanya vizuri katika soko ili kutengeneza faida ya kutosha," alisisitiza mwenyekiti huyo wa Bodi.
Hata hivyo alisema mabadiliko ya kimfumo na uendeshaji shughuli za mawasiliano ikiwemo kupunguza gharama za muingiliano wa mitandao (punguzo la 42%) yalioletwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesababisha kampuni hiyo kupunguza mapato yake na hata gawio kwa wanahisa kwa kiasi fulani tofauti na makadirio ya hapo awali ambapo Kampuni iliahidi kufanya vizuri na kutoa gawio la kuridhisha kwa wanahisa wake.
Mwenyekiti Ali Mufuruki ameongeza kuwa suala la usimamizi wa karibu wa Serikali kuhakikisha watumiaji wa simu za mkononi wanakuwa na usajili unaotambulika ipasavyo, nao umeiathiri kampuni katika matarajio ya kufanya vizuri katika eneo la mapato kwa kampuni na wanahisa wake.
Alisema lengo la kampuni ya Vodacom ni kuhakikisha inashinda katika soko na hata ukiangalia kwenye soko Vodacom ndiyo kampuni kubwa ya Simu Tanzania inaongoza kwa kiasi kikubwa wateja wa Vodacom wamekuwa wakiongezeka kila mwaka, hadi sasa tuna jumla ya wateja milioni 13.2 huku mwaka jana tulikuwa na jumla ya wateja 12.9 milioni.
Mkutano wa wanahisa wa Vodacom Tanzania umefanyika Mlimani City leo jijini na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanaahisa, ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa walipata fursa ya kujadili na kupitisha masuala mbaalimbali katika uendeshaji wa kampuni hiyo kubwa ya Simu nchini.
No comments:
Post a Comment