Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 3 October 2018

MASHIRIKA YA UNDER THE SAME SUN, CEFA TANZANIA NA GNRC TANZANIA, YAENDELEA KUELIMISHA JAMII KUHUSIANA NA UALBINO




  • Mradi wa HAKI YETU wakutana na Maafisa Maendeleo na ustawi wa jamii Kigoma na kuzungumza madhara ya kuwatenga watu wenye ualbino
  • Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii Kigoma wapigwa msasa uelewa kuhusu Ualbino
Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii, kutoka manispaa ya kigoma Ujiji wamehudhuria mafunzo ya uelewa kuhusu ualbino na elimu ya Amani na maadili iliyotolewa na mradi wa Haki Yetu mkoani Kigoma.

Mradi huu huu umekua ukiendeshwa tokea mwezi Aprili mwaka huu katika Mikoa ya kigoma na maeneo ya jirani kwa ushirika wa wadau Mbalimbali lengo lao likiwa ni kutoa msaada kwa jamii kuelewa zaidi kuhusu ualbino, kupunguza imani potofu, kuwajengea watu wenye ualbino misingi ya kujiamini ualbino pamoja na kutengeneza jamii shirikishi isiyokuwa na ma waa ya ubaguzi wa aina yoyote kwa watu wenye ualbini

Katika mradi huu misingi muhimu ambayo imekua ikiwekewa msisitizo ni pamoja na kuzingatia utu, kuwapa nafasi watu wenye ualbino bila kuwabagua, kushirikiana nao kwenye maswala ya elimu na uchumi lengo likiwa ni kujenga Taifa bora

Mradi wa Haki Yetu unatekelezwa na Mashirika ya Under The Same Sun, CEFA Tanzania na GNRC Tanzania, ukilenga kuelimisha jamii kuhusiana na ualbino.

No comments:

Post a Comment