Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devotha Mdachi naye akizungumza wakati wa maonesho yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi hiyo. |
Maonesho hayo ambayo yatafanyika kwenye miji mikubwa mitatau ya India yaani New Delhi, Ahmedabad na Mumbai yanalenga kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nnchini.
Akizungumza wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda alisema kuwa anaona fahari kubwa kushiriki maonesho hayo muhimu kwa Tanzania na India na alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kuanza wa safari za kwanza za ndege ya shirika la ndege la Tanzania mjini Mumbai.
Balozi Luvanda alisema kuwa safari za ndege hiyo nchini India ni fahari kubwa kwa Tanzania kutokana na ukweli kwamba nchi hizi mbili zina mahusiano ya kihistoria kwani mbali na kuunganishwa na Bahari ya Hindi, Tanzania na India ni marafiki na zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, utamaduni na mawasiliano ya mtu mmoja mmoja.
Mhe. Balozi Luvanda alisisitiza kuwa, safari za ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania nchini India hususan katika mji wa Mumbai zitaimarisha sekta ya utalii nchini kwa kuongeza idadai ya watalii kutoka nchini humo ambao kwa sasa takribani watalii 40,000 kutoka nchini humo wanatembelea Tanzania kwa mwaka. Pia zitarahisha safari za wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali vya India ambao idadi yao imeongezeka na kufikia 2500 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment