Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake (UN Women), Mhe. Bi. Phumzile Mlambo-Ngcuka anategemea kufanya ziara ya kikazi hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 24 Agosti, 2018. Ziara hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Shirika hilo na Tanzania.
Akiwa nchini, Bi. Mlambo-Ngcuka atahudhuria Mkutano wa Usawa wa Kijinsia,Malengo ya Maendeleo Endelevu na Vyombo vya Habari (Gender Equality, Sustainable Development Goals and Media Summit), utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti, 2018.
Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, Mkurugenzi huyo atatembelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na UN Women katika mkoa wa Dar es Salaam. Aidha, Bi. Mlambo-Ngcuka ataonana na viongozi wa kitaifa na viongozi wengine wa Serikali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
20 Agosti, 2018
No comments:
Post a Comment