Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 22 February 2018

MADEREVA DAR WAFURAHIA KUJIUNGA TAXIFY


Bajaji ni usafiri rahisi unaoweza kutumiwa na watu wenye vipato vya aina zote duniani.

Sababu kubwa ya usafiri huu kutumiwa na watu wengi ni gharama zake kuonekana kuwa ndogo na humpatia mtumiaji urahisi wa kufika sehemu anayoihitaji kwa haraka tofauti na gari.

Licha ya kuwa watu wengi wanaogopa kuzitumia kutokana na sababu za kiusalama na uendeshaji wa madereva wanavyo jipenyeza katikati ya magari kwenye barabara kubwa, lakini ni msaada mkubwa kwa wakazi waishio Jijini Dar es Salaam, jiji lenye msongamano mkubwa wa magari.

Kadhia hiyo ndiyo imeufanya usafiri huo kuwa maarufu kwa watu wengi na wa rika zote hasa wanapopata dharula, hulazimika kuacha usafiri wao au usafiri wa umma ili waweze kufika kwa haraka sehemu wanazohitajika.

Changamoto hiyo ya foleni imetumiwa kama fursa kwa Kampuni ya Taxify ambayo imezindua huduma mpya ya ‘Taxify Bajaji’ kwa lengo la kuwarahisishia wakazi wa Jiji la Dar es salaam kufurahia huduma za usafirishaji wa gharama nafuu na haraka.

Huduma hiyo ya kwanza kuzinduliwa nchini imekuja ikiwa ni miezi miwili tangu kuanzishwa kwa huduma ya Taxify iliyoweza kurahisisha upatikanaji wa taxi katika eneo lolote ndani ya jiji hilo.

Meneja wa Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika ya Mashariki, Shivachi Muleji alisema Taxify bajaji itasaidia kuunganisha watumiaji wa usafiri wa bajaji na madereva ndani ya dakika chache.

“Tumeamua kuanzisha huduma hii baada ya kugundua usafiri wa bajaji ni maarufu na unatumiwa na watu wengi wanaokwepa kukaa muda mrefu barabarani kutokana na foleni, kwa hiyo akipanda bajaji ataweza kupenya penya na kuwahi sehemu anayohitaji ndani ya muda mfupi,” alisema Mulaji.

Anasema uwapo wa huduma hiyo pia kunamsaidia mtumiaji kuchagua aina ya usafiri anaotaka kulingana na thamani ya fedha aliyonayo na uharaka wake.

“Madereva wa bajaji hawana tena sababu ya kuendelea kukaa vijiweni kwa muda wa saa mbili wakisubiri wateja, badala yake watakuwa na uwezo wa kufanya safari nyingi kwa siku,” anasema.

Kuna baadhi ya maeneo ambayo wateja walikuwa wakipata tabu ya usafiri kutokana na vituo vya daladaka kuwa mbali jambo linalowafanya kupoteza muda mwingi kutafuta usafiri.

“Wateja sasa watapata nafuu ya kupata usafiri kwa haraka kuliko ilivyokuwa kawaida,” anasema Muleji.

Anasema mpaka sasa wameshasajili madereva wa kutosha kukidhi mahitaji ya wateja.

Akizungumzia bei, taxify bajaji inatoza Sh750 hadi Sh350 kwa kilomita huku Sh75 kwa dakika wakati bei ya chini kabisa ikiwa ni Sh2,000.

Akizungumzia maendeleo ya huduma ya Taxify iliyoanzishwa miezi miwili iliyopita, Meneja mwendeshaji wa teknolojia hiyo nchini, Remmy Eseka anasema kumekuwa na ongezeko la asilimia 50 kwa madereva taxi waliojisajiri.
“Daima tunaangalia ni jinsi gani tunaweza kutoa ufumbuzi bora katika usafiri kwa ufanisi na mahitaji ya masoko mbalimbali ambako tunafanya kazi,” anasema Eseka.

Anasema teknolojia ndiyo kitu pekee kwa sasa kinachoweza kurahisisha upatikanaji wa kila kitu hasa huduma za usafiri.

Mmoja wa madereva ambao wamesajiliwa ili waweze kutoa huduma za usafirishaji kupitia Taxify Bajaji, Mohammed yusuph anasema anaamini ataweza kutengeneza fedha nyingi kupitia usafirishaji huo.

“Ni muda mrefu nimekuwa nikifanya kazi ya usafirishaji lakini haikuwa ya uhakika bali kwa kusubiria mteja kijiweni, lakini nafasi hii niliyoipata ya kuhudumia wateja sehemu yoyote ninapo kuwa itakuwa ni fursa kwangu ya kujiongezea kipato,” anasema Yusuph.

Anasema uwapo wa ajira hiyo itaweza kuinua maisha ya madereva wengi wa Jijini dar es Salaam kiuchumi.

“Hata ule muda wa kukaa kijiweni kusubiri wateja kwa saa mbili au kusubiri zamu yako utaisha na badala yake itakuwa ni kazi kazi tu,” anasema Yusuph.

Mwananchi

No comments:

Post a Comment