Dar
es Salaam, 6, Julai 2017 - Uber
imejitolea kutoa huduma ambayo ni rahisi na nzuri kwa abiria na madereva.
Sehemu ya kuunda uzoefu huu rahisi ni kutoa maelekezo kuhusu jinsi madereva na
abiria wanapaswa kufanya na kutendeana safarini. Hiyo ndiyo maana Uber imetoa Maelekezo yao yaliyosasishwa ya
Jamii, mwongozo huu sio tu wa
'jinsi ya' kwa madereva washiriki wa Uber, bali pia kwa abiria wa Uber.
Hii
ndio mara ya kwanza Uber imechapisha sera inayoelezea ni kwa nini abiria
wanaweza kupoteza uwezo wao wa kupata Uber. Hii ni muhimu kwa sababu wakati
madereva wanatumia Uber wanafanya zaidi ya kuendesha gari tu: wanashiriki gari,
nafasi na muda wao na abiria. Na ijapokuwa abiria wengi wanawaonyesha madereva
heshima, kwa bahati mbaya sio kila wakati.
Maelekezo
yaliyosasishwa ya Jamii ya Uber husaidia kuelezea ni nini Kisichokubalika
kwenye safari ya Uber. Nyingi kati ya hizi ni mambo ya kawaida kwa wengi wetu
lakini yanapaswa kuzingatiwa - iwe ni kutapika kwenye kiti cha nyuma au kuacha
takataka ndani ya gari, orodha iliyo hapa chini ya maelekezo ni moja ambayo
kila mtu anayetumia Uber anapaswa kuelewa - madereva na abiria na hata pia wale
wanaosafiri pamoja na abiria / marafiki wengine.
Lazima watoto waangaliwe.
Wale
walio chini ya umri wa miaka 18 wanaweza kutumia Uber wakisimamiwa na mtu
mzima, lakini hawawezi kuwa wenyewe na akaunti ya Uber. Wazazi au walezi
wanapaswa kuwa na watoto wao kila wakati.
Kwenda
mbele, ikiwa Uber itagundua kwamba mtoto asiyekuwa na mzazi ni mmiliki wa
akaunti, akaunti hiyo italemazwa mara moja. Kama Uber itagundua kwamba abiria
ana umri wa chini ya miaka 18 lakini mmiliki wa akaunti ni mtu mwingine ambaye
amezidisha umri wa miaka 18, Uber itamkumbusha mmiliki wa akaunti hiyo kuhusu
sera ya Uber na kulemaza wasifu wake baada ya onyo la pili.
Kufika
mwisho wa safari yako ndio kipaumbele cha juu. Hii ndio maana madereva
wanapaswa kutii sheria za barabarani kwa mfano, kufuata kasi inayoruhusiwa,
kutoendesha kama wamelewa au kutumia dawa na kutotumia simu wanapokuwa
wakiendesha gari. Madereva wanapaswa kupumzika kila wakati ikiwa wamechoka.
Abiria
wanapaswa kutekeleza jukumu lao la kuvaa mikanda ya viti na kutojaribu kuwabeba
watu zaidi wakati hakuna mikanda ya kutosha ya viti. Abiria wanapaswa pia
kujiepusha kubeba vileo au mihadarati ndani ya gari na hawapaswi kumwomba
dereva kwenda kwa kasi ya juu kuliko kasi inayoruhusiwa.
Wape abiria na madereva nafasi yao ya binafsi
Ijapokuwa
mazungumzo ya kirafiki hayana madhara yoyote wakati wa safari, heshima inapaswa
kudumishwa kila wakati. Abiria na madereva wanapaswa kupeana nafasi ya binafsi
na hawapaswi kufanya yule mwingine ajihisi vibaya. Uber ina sheria ya 'hakuna
vitendo vya kimapenzi', inayomaanisha hakupaswi kuwa na vitendo vya ngono kati
ya madereva na abiria. Hiyo ni pamoja na kuchezeana na kugusana. Migusano
yoyote ya kimwili kama vile kumgonga au kujaribu kumuumiza dereva yamepigwa
marufuku.
Heshima
Heshima
ni muhimu, hakuna wakati wowote abiria au madereva wanapaswa kutoheshimiana.
Magari yanayotumika kwenye app ya Uber ni ya madereva washiriki na wanajivunia
kuweka magari yao katika hali nzuri kwa ajili ya starehe ya abiria. Abiria
wanapaswa kuheshimu magari wanayoyatumia na wanapaswa kuacha magari hayo katika
hali ambayo waliyapata.
Tabia
ya ukaidi kama vile kuharibu gari haitakubaliwa. Kutumia lugha mbaya imepigwa
marufuku pia. Kuwa na fujo au ubaguzi kunaweza kusababisha abiria kupigwa
marufuku kutumia app hii. Uber haibagui kwa misingi ya jinsia au umbari na
abiria yeyote ambaye hashiriki mtazamo huu hakaribishwi kutumia app hii.
Maoni yanatusaidia sisi wote kuimarika.
Kutoa
maoni huwezesha Uber kujua abiria ameridhishwa au kutoridhishwa na nini, hiyo
ndio maana madereva na abiria wanapaswa kutoa maoni ya safari yao kila wakati.
Wakati watu wanajua kuwa wanatathminiwa wanakuwa makini zaidi kuhusu tabia zao
na wanawajibika kwa hatua zao. Ajali, ada isio sahihi ya nauli au mabishano
yanapaswa kuripotiwa kwa kubofya kitufe cha msaada kwenye app. Kuna timu ya
usaidizi kwa wateja ambayo iko tayari kusaidia kila wakati.
Baada
ya kujua kuhusu ukiukaji Uber itawasiliana na dereva ili kuchunguza. Kulingana
na hali ya tatizo, akaunti ya abiria inaweza kusitishwa kwa muda wakati wa
uchunguzi. Iwapo hoja hiyo itahusisha makosa makubwa yanayohusisha ukatili,
makosa kadhaa ya ngono, unyanyasaji, ubaguzi au shughuli ambazo ni kinyume cha
sheria, akaunti hiyo inaweza kulemazwa na mamlaka kufahamishwa. Uber itatoa
maelezo yoyote ambayo mamlaka itayahitaji ili kuwasaidia katika uchunguzi wao.
Uber
inajitahidi kuunda mazingira salama na mazuri kwa abiria na madereva washiriki.
Maelekezo haya ni muhimu na hutekelezwa kwa faida za wale wote ambao wanatumia
Uber. Madereva na abiria wanahimizwa kujifahamisha Maelekezo haya ya Jamii.
Kuhusu Uber
Misheni ya Uber ni
kuwasaidia watu kusafiri kwa kubofya kitufe tu - mahali popote na kwa ajili ya
kila mtu. Tulianza mwaka wa 2009 ili kutatua tatizo rahisi - unawezaje kusafiri
kwa kubofya kitufe? Miaka sita na zaidi ya safari bilioni mbili baadaye,
tumeanza kukabiliana na changamoto nyingine kubwa zaidi: kupunguza msongamano
na uchafuzi katika miji yetu kwa kuwabeba watu zaidi katika magari machache.
Mtandao wa Uber unapatikana
sasa katika zaidi ya miji 475 katika nchi 75 katika mabara 6. Ili kuomba
usafiri, lazima watumiaji wapakue app ya bure ya Android, iPhone, Blackberry 7,
au wajisajili kwenye tovuti ya Uber www.uber.com/go. Ikiwa una maswali tembelea
www.uber.com
Mtandao wa Jamii:
Twitter: @Uber_Tanzania | Facebook: /UberTanzania
|Instagram: @Uber_Tanzania
Kwa maelezo zaidi:
Janet Kemboi - Uber
Communications East Africa
Simu: +254 726390190
Barua pepe:
jkemboi@uber.com
No comments:
Post a Comment