Maafisa Wakuuu kutoka vitengo mbalimbali vya NMB wakifuatilia mkutano wa wanahisa. |
Mameneja wa kanda wa NMB kutoka kanda mbalimbali za benki ya NMB wakifuatilia Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa NMB. |
Benki ya NMB imeidhinisha shilingi Bilioni 52 kama gawio kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2014. Gawio hilo ni sawa na Shilingi 104 kwa kila hisa moja na ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka jana.
Gawio hilo ni kutokana na faida ya shilingi Bilioni 156 baada ya kodi iliyopatikana kwa mwaka 2014. Faida hiyo na gawio lililoidhinishwa ni Faraja kwa wanahisa wanaojivunia benki bora yenya matawi mengi kuliko benki yoyote Tanzania ikiwa na matawi zaidi ya matawi 163 na ATM zaidi ya 550 huku huduma zake zikiwa zimeenea kila wilaya hapa nchini.
Gawio hilo liliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi na kupitishwa na wanahisa katika mkutano mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment