Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA, Edward Greenwood akizungumza wakati wa kuzindua Benki ya FINCA jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya FINCA, Thabiti Ndilahomba akizungumzia kuhusiana na kutoa huduma bora kwa watanzania katika uzinduzi wa benki ya FINCA jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya FINCA. |
BENKI ya FINCA imewekeza kiasi cha sh. bilioni 22, ambayo imevuka kiwango cha masharti ya Benki Kuu ya Tanzania kwa uanzishwaji wa mabenki hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edward Greenwood wakati wa kufunga Taasisi ya mikopo kwa wafanyabiashara wenye kipato cha chini na kuzinduliwa Benki ya Finca katika ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 16 na kuendelea kuboresha huduma zao katika benki hiyo.
Greenwood amesema kuwa dhamira yao kubwa katika ufunguzi wa benki hiyo ni kupunguza ugumu wa maisha ya wananchi hapa nchini kwa kutoa kiwango kidogo zaidi kuliko ilivyozoeleka kwa taasisi zingine za kifedha ili kila mfanyabiashara aweze kufaidika na mikopo katika benki hiyo.
No comments:
Post a Comment