Benki ya Wananchi ya Dar es Salaam (DCB) imetoa mikopo yenye dhamani ya Sh.Bilioni 363.3 kwa wajasiriamali 362,507 kati ya hao wajasiriamali wadogo kupitia vikundi ni 156,718 katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Balozi Paul Rupia wakati wa kuwasilisha matokeo ya uendeshaji wa benki hiyo, amesema kipindi cha uendeshaji wa benki hiyo kwa mwaka miaka miwili, amana ilifikia sh.113 ikiwa ni asilimia tano za amana sh.bilioni 108 ambazo zilipatikana mwaka uliopita.
Rupia amesema mikopo kwa mwaka uliopita iliongezeka kwa asilimia tisa kutoka sh.bilioni 75 hadi kufikia sh.bilioni 82.4 kwa mwaka huu na mali zimeongezeka kwa asilimia 34 kutoka sh.bilioni 117 mwaka jana na kufikia sh.bilioni 157 mwaka huu.
Amesema faida zilizopatikana kwa mwaka uliopita ilikuwa ni sh.bilioni 3.77 baada ya kutolewa kodi ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia mbili ukilinganiasha na faida ya bilioni 3.71 iliopatikana mwaka 2013.
Rupia amesema katika mikopo yote iliotolewa na benki hiyo asilimia 80 ni wanawake ambao wanajishughulisha na ujasiriamali na idadi ya wanawake imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
No comments:
Post a Comment