Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 13 April 2015

BENKI YA NMB, AIRTEL WAZINDUA HUDUMA YA KIFEDHA KWA NJIA YA MTANDAO

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mh. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano akieleza jambo katika hafla hiyo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Borgjols akizungumza jambo.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia tukio.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel Sunil Colaso akizungumza jambo katika uzinduzi huo.
Viongozi hao wakishikilia bango lenye ujumbe wa uzinduzi huo wa Airtel Money na benki ya NMB.
Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja na bango lenye ujumbe wa uzinduzi huo.
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel wamezindua huduma ya kuweka na kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za wateja kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money kupitia simu zao.

Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, aliyesisitiza umuhimu wa huduma hiyo katika kuleta maendeleo ya taifa.
Alisema ushirikiano baina ya vyombo hivyo viwili ni muhimu na serikali inaunga mkono maana utaleta mageuzi katika maisha ya watanzania pamoja na maendeleo kwa ujumla .

“Kwa niaba ya serikali, napenda kuishukuru benki ya NMB pamoja na kampuni ya simu ya Airtel kwa kuingia katika ushirikiano huu uliosubiriwa kwa kipindi kirefu na wananchi, kampuni hii kubwa ya simu na benki inayoongoza kuwa na mtandao mkubwa wa matawi na mashine za ATM nchini, utatoa nafasi itakayokuza huduma za kifedha nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel Sunil Colaso alisema kuwa umoja huo ni ishara tosha ya kuonesha mageuzi katika matumizi ya teknolojia katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia simu zao za mkononi.

Alisema kuwa huduma hiyo ya kibunifu itawawezesha kufanya miamala ya kifedha kirahisi, kwa njia salama kupitia simu zao za mkononi na kuboresha huduma wakati wowote, popote walipo hasa ukilinganisha na wakazi wengi wa vijijini ambako benki zilikuwa mbali na mahitaji yao.

"Kwa njia hii wateja wa Airtel na NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB hata pia mteja anaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money,’’ alisema Colaso.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa NMB, Tom Borgjols alisema kuwa uzinduzi wa huduma ya Airtel Money kwa huduma ya simu ya NMB mobile ni sahihi kwani itawawezesha watu wasio na akaunti na ambao hawajatimiza vigezo vya kufungua akaunti na wenyewe kupata huduma za kifedha karibu yao.

Alisema kuwa uzinduzi wa huduma hiyo uliounganishwa na NMB mobile utawawezesha wateja zaidi ya 1,000,000 waliojiunga na huduma hiyo kupata kuweka na kutoa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda katika akaunti zao za NMB ikiwa ni kwa bei nafuu.

Naye mwongozaji wa Huduma ya kutoa na kuweka fedha katika akaunti ya simu za mkononi ya Airtel Money, Aijaz Khan alisema kuwa mteja wa huduma hiyo anaweza kuandika herufi *150*60# na kufuata maelekezo ambayo yatamuongoza katika kupata huduma anayohitaji.

(PICHA/STORI NA DENIS MTIMA /GPL)

No comments:

Post a Comment