Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini amezindua usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua, Rex Energy, inayotarajia kuzifikia kaya milioni moja na nusu kufikia mwaka 2020 kupitia teknolijia mpya ya umeme wa jua wa gharama nafuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia hiyo mpya inayojulikana kama 3G+ Solar Home System (SHS) iliyobuniwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ikiwa ni mara ya kwanza kutumika Tanzania, Mkurugenzi Mtendai wa Rex Energy Francis Kibhisa lengo la mradi huo ni kuwafikia watanzania wengi zaidi
Teknolojia hiyo ya kisasa imebuniwa na mshirika wa Rex Energy, Kampuni ya Nishati ya Solaric Pvt Ltd yenye makao makuu nchini Bangladesh.
Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa teknolojia hiyo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Rex Energy, Francis Kibhisa alisema; “Rex Energy imefanikiwa kuwa mbele katika utoaji wa bidhaa bora zilizo suluhu ya soko la nishati ya jua na kwa kuzindua 3G+SHS leo, nawahakikishia wateja wetu bidhaa bora ya SHS kwa mahitaji yao ya jumla.”
Teknolojia hii imejaribiwa nchini Bangladesh, India na Malaysia na nina uhakika ni suluhisho kwa maeneo yasiyofikiwa na gridi vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa mpango wa muda wa kati,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Bangladesh alisema: “Kwa uvumbuzi wa 3G+SHS, gharama za SHS zimepunguzwa na kadhalika mahitaji ya kuihudumia kwa kiasi kikubwa na kuifanya bidhaa hiyo kuwa yenye faida kibiashara.”
“Rex Energy iliteuliwa kuwa mshirika wetu kwa sababu ya rekodi yao nzuri katika sekta ya nishati ya umeme wa jua na uwezo wao wa kulifikia soko,” alisema.
Uzinduzi wa 3G+SHS pia unatoa suluhu ya masuala ya kuimudu bei, ambayo yamekwamisha watu wengi walio nje ya umeme wa gridi kunufaika na nishati.
“Tuna mfumo wa malipo, ambao unaruhusu wateja kulipa amana na kiasi kilichosalia kulipwa kipindi cha miezi 12 ili kumsaidia mteja kutobeba mzigo wa kulipa mara moja,” alisema.
“Huu ni mfumo wa lipa kadiri ya unavyotumia (PAYG), ambao mteja anamiliki mfumo wa umeme wa jua baada ya kumaliza kulipa sehemu ya fedha iliyobakia. Bidhaa pia imetengenezwa kwa namna ya kuendana na mahitaji ya makundi tofauti ya jamii za vijijini na hata za mjini kwa vile inakuja kwa ukubwa tofauti linapokuja suala la uwezo wa nishati ukihusisha kuanzia matumizi ya mwanga na kuchaji simu hadi kuwezesha vifaa vya umene kama vile runinga; feni, kompyuta mpakato na kadhalika,” Kibhisa anasema
Akifafanua kuhusu kufanya uzinduzi huo kwa wakati huu, Mkurugenzi huyo Mkuu wa Rex Energy alisema, “Rex Energy imejitoa kwa ajili ya kusaidia juhudi za serikali za kupeleka umeme katika maeneo magumu kufikika, maeneo yaliyo nje ya gridi na masoko mengine yanayokabiliwa na ukosefu wa usambazaji wa umeme wa uhakika. Uzinduzi haungeweza kuja kwa wakati mzuri kuliko huu sasa.
“Hii ni sehemu nzuri ya kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania kupitia Mpango wake Kamambe wa Umeme wa kutoa umeme kwa idadi kubwa ya watu wa vijijini ifikapo mwaka 2030. Rex Energy imepanga kutoa teknolojia ya umeme ya 3G+ SHS kwa kaya karibu milioni 1.5 ifikapo mwaka 2020,” Mkurugenzi huyo alisema.
Mradi huu utashuhudia ajira karibu 2, 500 zikitengenezwa katika mchakato huo, ukinufaisha vijana wa ndani, ambao watapewa mafunzo na Rex Energy kuwa mafundi wa kuweka mfumo wa umeme wa jua na au kutoa huduma za mauzo chini ya usimamizi wa mafundi sanifu wa Rex Energy.
Hali kadhalika mawakala wapya watahusishwa kwa ajili ya usambazaji wa 3G+SHS katika mikoa tofauti ya Tanzania huku ajira zaidi zikitarajiwa kupitia miradi ya wajasiliamali wa ndani waliowezeshwa.
Katika hotuba yake, ………… ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa mwito kwa sekta nyingine binafsi, Taasisi Zisizo za Kiserikali na washirika wa maendeleo kuungana na juhudi za serikali katika utekelezaji wa sera, kwa ajili ya maendeleo jumuishi na endelevu.
“Hii ni kazi yetu sote tukiwa na lengo moja la kutoa nishati ya jua katika jamii za vijijini na kwa kufuata mfano uliooneshwa leo hii na Rex Energy, umasikini katika jamii za vijijini nchini Tanzania utakuwa historia,” alisema.
Father Kidevu
No comments:
Post a Comment