Tido Mhando
|
Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Tabata, Dar es Salaam.
Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.
“Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera BBC, na kwa kuwa za kwetu ni mpya, zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,” amesema.
Tido amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo, zoezi la uzinduzi wake rasmi litafanyika kesho, asubuhi mjini Dar es Salaam.
Mhando ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu enzi zake nchini kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
“Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho, ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam TV,” alisema Tido.
Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment