Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 30 March 2015

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA MAFUTA, KOFIA, PIKIPIKI NA KOMPYUTA KWA MAALBINO

Mkuu Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Musa Jallow (wa tano kulia) akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, kompyuta, kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Ofisa Mkaguzi wa Sheria za Ndani za Benki wa NBC, Lilian Kawa (katikati) akikabidhi msaada wa kofia kwa Katibu wa Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Aicha Joakim Ngure (wa tatu kushoto) katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na mafuta maalumu ya ngozi ili kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na tatizo unaotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mafuta maalumu ya ngozi kwa mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na kofia vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja Udhibiti wa Sheria wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanakombo Joshua (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa kampyuta kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki , kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Ofisa Uchunguzi wa Idara ya Udhibiti wa Sheria wa Benki ya NBC, Mathias Raymond (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa kompyuta kwa mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kofia na mafuta ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Sheria wa NBC, Joyce Mbago (wa tatu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 3.2 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa pikipiki , kofia, kompyuta na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC, wakiwa na wawakilishi wa Chama cha Albino Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment