Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 31 March 2015

BENKI YA NBC YASOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI KARIBU ZAIDI KWA WATEJA KWA KUZINDUA 'NBC BENKI NILIPO' JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Maria Alina Kimaryo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto) na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph wakizindua huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia program maalum ya NBC katika ‘play store’ hivyo kupata huduma za kibenki kupitia laptop zao, tablets na simu za mkononi za smartphones.
Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canicius Joseph (kulia), akionyesha jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.
Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (katikati) akimwonyesha mmoja wa mteja, Nusra John (kulia) jinsi anavyoweza kutoa pesa katika ATM ya benki hiyo bila ya kuwa na kadi kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.
Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph.
Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canicius Joseph (kulia), akimwonyesha mmoja wa wateja, Amini Juma (kushoto), jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakishuhudia uzinduzi wa NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment