Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Thursday, 24 November 2022

NAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA BURUNDI AIPONGEZA BENKI YA CRDB BURUNDI KWA MIAKA 10 YA MAFANIKIO

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wa tatu kulia) akikabidhi tuzo maalumu ya shukrani ya maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi kwa Naibu Gavana wa kwanza Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse (katikati) pamoja na Naibu Gavana wa pili, Marie Goreth Ndayishimiye. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba (wa pili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Burundi, Fredrick Siwale (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Menard Bucumi.

Bujumbura, 24 Novemba 2022 - Benki Kuu ya nchini Burundi (BRB) imeipongeza Benki ya CRDB Burundi kwa mafanikio makubwa iliyopata katika kipindi cha miaka 10 ya uwepo wake nchini Burundi.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Burundi kwa niaba ya Gavana katika mkutano na ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na wajumbe wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB pamoja na kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi. Ujumbe huo umetembelea Benki Kuu ya Burundi kutoa shukrani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma za kibenki ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi.


Akizungumza katika mkutano, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse alisema Benki Kuu ya nchi hiyo inafurahia sana kwa uwepo wa Benki ya CRDB nchini Burundi kwani imekua sehemu ya uwezeshaji wa miradi mingi ya kiuchumi kwa nchi lakini pia imechangia uwezeshaji wa wafanyabiashara.

“Tulipata matatizo yaliyopelekea changamoto kubwa ya upatikanaji wa fedha za kigeni mwaka 2015 lakini tulipata msaada mkubwa sana kutoka Benki ya CRDB na hakika hilo limedhihirisha ule usemi wa rafiki wa kweli hujulikana wakati wa shida” alisema Musharitse.


Tangu ilipoingia katika soko la Burundi mwaka 2012, Benki ya CRDB imekua ikifanya vyema sokoni na katika kipindi cha miaka 10 tu imeweza kushika nafasi ya tatu kati ya benki kumi na tatu zinazotoa huduma za kibenki nchini Burundi. Katika kipindi hiko Benki imeweza kufungua matawi manne huku tawi la tano likitarajiwa kufunguliwa mapema mwaka 2023.

“Kutokana na kufanya vizuri kwa Benki ya CRDB Burundi tunatamani kuona ikifungua matawi mengi zaidi nje ya Bujumbura lakini pia kuweza kufanikisha upatikanaji wa mikopo kwa njia za kidigitali kama ambavyo wamekua wakitoa huduma nyingine kidigitali” aliongeza Musharitse.


Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameishukuru Benki Kuu ya Burundi kwa ushirikiano mkubwa kwa Benki ya CRDB Burundi uliopelekea kampuni tanzu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi cha miaka 10. Sambamba na hilo Nsekela ameishukuru Serikali ya nchi hiyo chini ya Rais Evariste Ndayishimiye kwa kuipatia eneo Benki ya CRDB Burundi katika makao makuu mapya ya nchi ya Gitega ili kufanikisha ujenzi wa tawi jipya.

DKT. MWIGULU ATETA NA MKURUGENZI WA CITIBANK

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank, David Livingstone, walipokutana na kufanya mazungumzo, Ofisi ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb), akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank, David Livingstone (hayupo pichani) ambapo Mkurugenzi huyo aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank, David Livingstone ambapo Mkurugenzi huyo aliahidi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, jijini Dar es Salaam. Kikoa hicho kimehudhuriwa na Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe wa Citibank.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa nne kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank, David Livingstone (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe kutoka Citibank baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwingulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Citibank Unaosimamia Ukanda wa Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati, ambapo benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji na kufanya tathimini ya uwezo wa`nchi kukopesheka (credit rating).

Dkt. Nchemba amefanya kikao jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group, David Livingstone amesema Benki yake inajivunia kufanyakazi na Tanzania katika kufikia agenda yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mhe. Dkt. Nchemba alielezea kuwa wamejadiliana namna ya kuharakisha ukamilishaji wa suala la tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka katika masoko ya kimataifa (credit rating) ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo CITI Group ndio washauri wakuu wa zoezi hilo.

NMB BANK PLC - 18 AWARDS AND COUNTING!






We are proudly ending 2022 with a trail of 18 awards from reputable national and international institutions that collectively recognize us as the Best Bank in Tanzania. Among the accolades, some recognize our CEO, Ruth Zaipuna as the Best Banking CEO in Tanzania which emblems her strong leadership of our Bank.

Below is a complete list of awards NMB Bank Plc won in 2022:

✅ The Best Bank in Tanzania 2022 from Global Brands Magazine
✅ Best Retail Bank from International Business Magazine
✅ Best Retail Bank from Global Banking & Finance Review
✅ Best Retail Bank from World Economic Magazine
✅ Best Agri Business Bank from Global Brands Magazine
✅ Best Innovation in Retail Banking in Tanzania from International Banker Awards
✅ Best Private Bank in Tanzania from International Banker Awards
✅ Platinum Winner Sustainable Bond of the Year from Global Small and Medium Enterprises (SMEs) Finance Forum Awards
✅ Best Banking CEO Tanzania from Global Brands Magazine
✅ Best Banking CEO Tanzania from World Economic Magazine
✅ African Business Leadership Commendation Award 2022 - The Africa Summit
✅ African’s Banking CEO of the year 2022 (Tanzania) from Africa Bank 4.0 Awards
✅ Bank CEO of the Year – Financial Women Awards
✅ Overall, Winner – National Most Compliant taxpayer – Tanzania Revenue Authority
✅ Most Complaint Taxpayer in the Banking sector Tanzania – Tanzania Revenue Authority
✅ Third Winner : Outstanding Tax Contribution 2021/2022 - Tanzania Revenue Authority
✅ Africa’s First Bank to Earn an EDGE Certificate for Gender Equality
✅ Honorary Fellowship Award – Tanzania Institute of Bankers

We thank our employees, customers, regulators and all stakeholders who have been instrumental towards our bank’s success.

#NMBCloseToYou

NMB YANYAKUA TUZO 18 ZA UBORA - KITAIFA NA KIMATAIFA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB, Benson Mahenya moja ya tuzo 18 za kitaifa na kimataifa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NMB, Ramadhan Mwikalu na kulia ni Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NMB wakiwa na Menejimenti ya NMB, katika picha ya pamoja wakiwa na baadhi ya tuzo ilizoshinda benki hiyo, baada ya kuzitangaza kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya NMB.
Baadhi ya Tuzo kati ya 18 za kitaifa na kimataifa ilizotunukiwa Benki ya NMB.

Benki ya NMB imedhibitisha uongozi na sifa yake ya kuwa taasisi kinara wa huduma za kifedha nchini na isiyo kuwa na mpinzani, katika kulihudumia taifa baada ya kutwaa tuzo 18 za ubora za kitaifa na kimataifa.

Benki hiyo itametangaza kuwa, tuzo 10 za kimataifa imetunukiwa hivi karibuni kwa kuwahudumia vyema wateja wake na watanzania wote kwa ujumla, pamoja na kuwa kinara wa ujumuishaji wa kifedha nchini. Nne kati ya tuzo hizo, zimetolewa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Ruth Zaipuna kwa kuwa kiongozi bora.

Akizungumza katika hafla ya kuzitangaza tuzo hizo, Ruth alizitaja baadhi ya tuzo hizo kutoka kwenye majarida ya kimataifa zikiwa ni pamoja na:
  • Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2022 - Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
  • Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara - Kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la International Business Magazine na Jarida la Global Banking and Finance Review
  • Benki Bora katika Kilimo Biashara - Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
  • Ubunifu Bora katika Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi Tanzania - Kutoka International Bankers Award
  • Benki Bora kwa Wateja Maalum - kutoka International Bankers
  • Afisa Mtendaji Mkuu Bora kwa Mabenki nchini Tanzania - kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la Global Brands Magazine na African Bank 4.0 Summit
  • Hatifungani Bora ya Mwaka 2022 - kutoka Mtandao wa Mitaji kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati ambao wameshirikiana na nchi za G20 na IFC.

Wednesday, 23 November 2022

KIVUMBI CHA KOMBE LA DUNIA 2022 NDANI YA DStv



Kivumbi cha kombe la Dunia 2022 kinaendelea kutimka!

Jumatano ya leo Ujerumani watavaana na Japana, je kwa namna zilivyo timu hizi, tutegemee matokeo yapi?
@georgeambangile

Mechi hii huipati popote isipokuwa @dstvtanzania, lipia sasa kifurushi cha Compact ili kutazama mechi hii Live!

#HiiNiKwaKilaShabiki

BOA BANK BOARD CHAIRMAN - NEHEMIAH MCHECU MAKES OFFICIAL VISIT TO BANK OF TANZANIA

Bank of Africa Tanzania Chairman - Nehemiah Mchechu (left) and Managing Director - Adam Mihayo (second left) share a light moment with Bank of Tanzania Deputy Governor: Financial Stability and Deepening - Sauda Msemo and Director of Financial Sector Supervision - Sadati Musa, after a meeting which focused on how Bank of Africa Tanzania is supporting financial inclusion and the economic development agenda in Tanzania.


SERENGETI BREWERIES LAUNCHES MASSIVE EXPANSION OF BREWERY FACILITY IN MOSHI



Moshi, 22 November 2022 - The Government of Tanzania and Serengeti Breweries Limited (SBL) took part in the launch of the Serengeti Brewery, Moshi branch expansion today, Tuesday, November 22, 2022 in Moshi. Hon. Exaud Silaoneka Kigahe, Deputy Minister of Industry, Trade and Investment, who attended the event as a Guest of Honor, stated that the expansion of this facility is significant because it shows the level of investment SBL continues to make in the country to increase its productivity and accelerate economic growth by providing employment opportunities for local farmers to get market for their produce.



Addressing the media in Moshi, the Deputy Minister commended SBL for the state-of-the-art machinery and equipment that are operated with modern technology. “The Government is very happy with the investment Serengeti Breweries has made in the industry. Again, we recognize that this investment comes at a time where our Government, led by President Samia Suluhu Hassan, is working to reduce bureaucracy in investment and provide great incentives for investors to come to Tanzania because it is the right country with attractive policies and a wide range of investment opportunities. When more companies like SBL continue to invest our people get employment opportunities and farmers which is a big economic driver in Tanzania are able to get market for their produce" he said.



"The SBL company has made a significant contribution to the country's economy by creating many jobs and paying taxes that support our country's budget; again, your contribution in uplifting farmers by purchasing their produce is exemplary; and your participation in various social activities in this country is commendable at all times." he added



The expansion of the Serengeti Brewery facility in Moshi is part of SBL's three-year investment in expanding the business, which has cost approximately 185 billion shillings in capital expenditure. Between 2019 and 2020, 31 billion shillings were invested in the Dar es Salaam brewery; 13.4 billion shillings in the construction of the spirits production facility; and 124 billion shillings in the expansion of the beer production facility in Moshi, which will take place between 2021 and 2022. Last year, we spent another 15.7 billion shillings to expand our Mwanza brewery.

Tuesday, 22 November 2022

NMB HAKUNA KUPOA! TUPATE MUBASHARA KESHO SAA 4


Kesho mapemaaa tunaenda kuandika historia. 

Usikose, tufuatilie live kupitia mitandao yetu ya kijamii!

#NMBKaribuYako

SERENGETI BREWERIES LAUNCHES “ROCKSHORE” - FIRST INTERNATIONAL PREMIUM FLAVOURED BEER



Serengeti Breweries Limited (SBL), has introduced a new international premium beer called “Rockshore” from the House of Guinness for the expressive and lifestyle consumers.


Rockshore, a beer of international standards and locally produced, comes to the market as a response to the evolving tastes of Tanzania beer consumers looking for exclusive and premium taste. The beer has natural fruit flavours of vibrant pineapple and zingy passionfruit with an Alcohol by Volume (ABV) of 4.2 percent.



SBL’s Head of Innovation, Bertha Vedastus, during the trade launch, said “We are seeing a growing middle-class society across different age segments who seek options out of the norm, seeking freedom and expression beyond the rulebook. SBL is responding to these consumers by introducing Rockshore; a beer that allows them “to be unapologetically expressive gives you power to play by our own rules and just be free".



Speaking at the trade launch, the Marketing and Innovations Director, Anitha Msangi Rwehumbiza said “We continue to listen to our consumer evolving needs and respond accordingly with different products that answers to those needs. Rockshore is an innovative addition to our beer brands”.

BENKI YA NCBA YATOA PIKIPIKI MPYA KWA WASHINDI WA KAMPENI YA 'CHUZI LIMEKUBALI'

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya NCBA, Peter Kimweri akiwa na washindi - Martin Simbeye (wa pikipiki) na Zebedayo Mwasongole (wa Milioni 5). Pembeni ya washindi ni Fredrick Limbeghala - Mkuu wa Kitengo cha Benki Kidijitali pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo.


Dar es Salaam, tarehe 19 Novemba 2022 - Benki ya NCBA kwa mara nyingine tena, na kwa raundi ya mwisho katika 'Chuzi limekubali', yatoa pikipiki mpya kabisa kwa washindi wakuu wa kampeni yao ya M-Pawa. Mara hii hafla hiyo ilifanyika katika soko la Tegeta Nyuki tarehe 19 Novemba, 2022.



Kampeni hio yenye mafanikio makubwa inadaiwa pongezi zake kwa ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za mitandao ya simu nchini, na benki ya NCBA, ambayo hivi karibuni imetangazwa kuwa Benki Bora ya Kidijitali ya mwaka 2022 nchini Tanzania kwa Mapitio ya Fedha na Global Magazine.



Peter Kimweri, Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani katika benki ya NCBA, alisema kuwa kampeni hii imekuwa juhudi za mabadiliko ya tabia ili kuhimiza Watanzania kuchukua tabia sahihi za kuweka akiba na ulipaji wa mikopo mapema."Tumeona kazi hii kwa manufaa ya benki na hasa wateja wetu. Kupitia M-Pawa wanapata mikopo papo hapo na kupitia marejesho yao kwa wakati wanaweza kupata ukuaji wa riba mara kwa mara ili kumudu kuwapa mikopo zaidi kwa riba ndogo." Alisema.

WAZIRI WA NISHATI MHE. MAKAMBA AZINDUA DUKA LA VIFAA VYA DIGITALI - GADGET SHOP, SEA CLIFF MASAKI



Kwenye uzinduzi Gadget Shops Mega Store iliudhuliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. January Makamba alikua ndio mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi akiongea wakati wa uzinduzi alisema “Leo tumekuja kumuunga mkono rafi yangu Zelfa kwenye duka hili la Gadget Shop ni duka ambalo linauza vifaa vya electroniki, kama simu, kompyuta, TV, friji, vifaa vya game na kadhalika ni duka kubwa kabisa ambalo amelipanua alikua kwenye kachumba kadogo saivi amekuja kwenye sehem kubwa zaidi.


Tumekuja kumuunga mkono na kumpongeza sisi tunaamini kabisa kwamba moja ya changamoto apa nchini ni vifaa vya kielektroniki ambavo havina ubora vinachukua muda mfupi kuharibika inavojitokeza maduka kama haya au wauzaji kama hawa wanauza vifaa vyenyewe kabisa orijino sio kuuza tu wanatoa huduma za kiufundi kwa maana hiyo mteja anapata thamani ya pesa alioitoa kabisa na duka likipanuka kama hivi watu wengi wanapata kazi zaidi, wanauza zaidi na wanalipa kodi zaidi.


Kwaiyo ni kitu kizuri, tumekuja kumuunga mkono. Mimi siku zote nimekua nikinunua vitu kwake simu, charger na kadhalika nilivosikia kafanya jambo akanialika nimekuja kumuunga mkono na kumpongeza na imani yangu mafanikio yake yatakua zaidi.” 



Hili ni duka la huduma moja kwa kila aina ya vifaa vya ubunifu, vifaa vya kielektroniki, kompyuta, vifaa vya michezo ya Kubahatisha, simu za ganja na bidhaa za zawadi.

Gadget Shops Mega Store limefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 18 Novemba 2022.



Tukio la uzinduzi huo lilifanyika Sea Cliff Masaki. Wageni walipata fursa ya kujionea uzinduzi huo na kuwa wa kwanza kufanya manunuzi kwa bei nafuu.”

Kwa uzoefu wa miaka saba, utaalam wetu unajua jinsi ya kuhakikisha ubora katika duka la Gadget TZ, kutoka kwa huduma inayotolewa hadi kwa bidhaa yenyewe kwani tunalenga kuongeza uzoefu kwa duka moja linalotoa bidhaa zote, halisi na kwa hiyo kutengeneza fursa za ajira endelevu kwa watanzania wengi katika mnyororo wa thamani ya biashara yetu.

Kwa Mawasiliano:
Website: www.gadgetshop.co.tz
Instagram: @gadgetshop_tz
WhatsApp: 0799 788 887

TANGA CEMENT KIDEDEA WAZALISHAJI BORA TUZO ZA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akikabidhi Tuzo za 16 za Rais za wazalishaji bora wa Viwandani (PMAYA), kwa mshindi wa jumla ya wazalishaji bora wa mwaka 2021 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement wazalishaji wa Simba Cement (TCPLC), Reinhardt Swart, wakati wa hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam. Tanga cement iliibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa jumla na kuwa mzalishaji Bora. Wengine pichani ni Maofisa kutoka Tanga Cement.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akikabidhi Cheti cha Udhamini wa Tuzo za 16 za Rais za Wazalishaji Bora wa viwandani (PMAYA) kwa Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement, Mtanga Noor pamoja na Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko ambapo Tanga Cement waliibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa jumla na kuwa mzalishaji Bora wa Makampuni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement wazalishaji wa Simba Cement (TCPLC), Reinhardt Swart, pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanga Cement wakiwa katika hafla hiyo.

UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 210

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisaini nyaraka za makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 210 ambazo Ujerumani imeipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya sekta za afya, maji, utalii, mazingira, utawala bora, kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuboresha mfumo wa kidijitali kwa ajili ya kufuatilia matukio ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto. Kulia ni Naibu Waziri anayesimamia uhusiano wa kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Barbel Kofler.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya msaada wa shilingi bilioni 210 ambazo Ujerumani imeipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya sekta za afya, maji, utalii, mazingira, utawala bora, kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuboresha mfumo wa kidijitali kwa ajili ya kufuatilia matukio ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban na kulia ni Naibu Waziri anayesimamia uhusiano wa kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Barbel Kofler.

Ujerumani imepatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 210 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya sekta za afya, maji, utalii, mazingira, utawala bora, kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuboresha mfumo wa kidijitali kwa ajili ya kufuatilia matukio ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Ujerumani imetangaza uamuzi huo mjini Berlin baada ya kukamilika kwa majadiliano kati ya ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Ujumbe wa Ujerumani ulioongozwa na Naibu Waziri anayesimamia uhusiano wa kiuchumi na Maendeleo wa nchi hiyo, Dkt. Barbel Kofler.

“Serikali ya Tanzania inafuraha kupokea msaada wa Euro milioni 87 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 210, utakaosaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha Maisha ya watu” alisema Dkt. Nchemba wakati akitoa neno la shukrani baada ya kusainiwa kwa nyaraka za makubaliano ya msaada huo.

REQUEST FOR EXPRESSION OF INTEREST TO INVEST IN NHC PLOTS THROUGH JOINT VENTURE ARRANGEMENTS


AFRICACOM 2022: HUAWEI LAUNCHES TRANSFORMATIVE FINTECH OFFERING TO REVOLUTIONIZE MOBILE MONEY


Cape Town, 18 November 2022 - Huawei last week announced the launch of an innovative fintech offering, which is set to revolutionize mobile money in Africa, aiming to increase financial inclusion and greatly improve the consumer’s digital user experience.

Called Fintech 2.0, the product was announced at AfricaCom, Africa’s largest technology gathering.

The solution will also empower micro, small, and medium-sized enterprises (MSMEs) to digitally transform, and provide service providers with greater business agility. In doing so, Huawei believes it will accelerate industry innovation and digital financial inclusion in emerging markets.

Fintech 2.0 brings value to mobile fintech operators through an extremely digital experience, accelerated innovation, and expedited time to market. In terms of digital experience, the solution’s digital architecture allows operators to ensure that the overall experience is tailored to every aspect of a customer’s life and combines simple and fast payment and lending.

Additionally, it allows for accelerated innovation by simplifying application development for MSMEs. Developers are able to reuse available industry assets including custom templates and components to rapidly build service applications using the best visual tools with minimal coding.