Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Friday, 16 May 2025

PUMA ENERGY, AMEND WASHIRIKIANA KUELIMISHA WANAFUNZI KUPITIA MAHAKAMA KIFANI YA WATOTO

Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kibugumo ya Kigamboni, Munir Said Mussa (12), katikati, akimhoji mmojawapo wa dereva aliyekamatwa nje ya barabara karibu na shule hiyo katika ‘Mahakama Kifani ya Watoto’ kwa kukiuka alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’ inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na shirika la Amend nchini.

Katika kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani Duniani (May 12 - 18, 2025), kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Amend Tanzania wameendesha 'Mahakama Kifani ya Watoto' kuhusu usalama barabarani tukio ambalo ni sehemu muhimu ya programu ya kampeni ya elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi ambayo pia inajulikana kama ‘Be Road Safe Africa’. Tukio hilo lilifanyika katika Shule ya Msingi ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kuanzia mwanzoni mwa wiki na kuhitimisha siku ya Ijumaa ya Mei 16.


Awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘Be Road Safe Africa’, ilitekelezwa mwaka 2023 na 2024, ambapo iliwafikia watoto zaidi ya 38,000 katika shule 20 za nchini Tanzania, Botswana, Zambia, na Zimbabwe. Awamu ya pili itatekelezwa katika nchi za Tanzania, Botswana, Zambia, Zimbabwe, na Afrika ya Kusini. Kwa nchini Tanzania awamu hii imezinufaisha shule tano ambazo ni: Kisukuru (Tabata), Kunguru (Goba), Mjimpya (Kurasini), Ufukoni (Kigamboni), na Salasala (Salasala).


Kampeni ya mwaka huu imewafikia zaidi ya wanafunzi 6,960 kupitia njia rahisi na shirikishi za kujifunzia, ikiwemo simulizi za hadithi, michezo - inayohusiana na masuala ya usalama barabarani na ‘Mahakama ya Watoto’. Wakati wa mahakama hii, wanafunzi hujifanya kama ‘majaji wa usalama barabarani’ ili kuwasaidia madereva kuelewa umuhimu wa kuzingatia usalama. Cha kuvutia zaidi, zaidi ya wanafunzi 290 wa chekechea pia walikuwa miongoni mwa wanufaika wa elimu ya usalama barabarani kupitia mpango huo.


Katika vifo 31 kwa kila watu 100,000, WHO inaripoti kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini Tanzania ni karibu mara 1.7 ya kiwango cha kimataifa na juu zaidi ya wastani wa Afrika. Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania zinaonyesha kuwa mwaka 2024 pekee, nchi ilirekodi ajali 1,735 za barabarani ambapo ajali 1,198 kati ya hizo zilisababisha vifo vya Watu 1,715. Makosa ya kibinadamu, ikiwemo kupuuzia alama za barabarani, kuendesha gari kwa uzembe, na mwendokasi, vilichangia 97% ya matukio haya.



Programu ya ‘Be Road Safe Africa’ ni sehemu ya dhamira ya Puma Energy Tanzania ya kusaidia usalama na ustawi wa jamii, hasa jamii zilizo katika mazingira magumu na maeneo hatarishi. Kupitia mafunzo ya mbinu mbalimbali, mashindano, na uboreshaji wa miundombinu, programu hii inasaidia kuzifanya barabara zetu kuwa salama kwa watoto wa shule nchini.

NBC YAKABIDHI KOMBE LA UBINGWA WA "NBC CHAMPIONSHIP" KWA MTIBWA SUGAR FC

Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar FC, viongozi na wadau mbalimbali wakijipongeza baada ya timu hiyo kukabidhiwa rasmi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) msimu wa 2024/2025. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya kirafiki kati ya bingwa huyo na timu ya Mbeya City FC mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 2-2.
Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) akikabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (kushoto) ili aweze kulikabidhi kwa nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar FC, Oscar Masai (kulia) baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa ligi ya NBC Championship msimu 2024/2025.
Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (kushoto) akikabidhi kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kwa nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar Oscar Masai baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025.
Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto (alievaa kanzu) akiongoza zoezi la uvalishaji wa medali kwa wachezai wa Mtibwa Sugar FC walioibuka mabingwa wa kombe la Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) msimu wa 2024/2025.
Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) akiwapongeza wachezaji wa timu ya Mbeya City wakati wa hafla hiyo.

Dar es Salaam, Mei 16, 2025: Mdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Mtibwa Sugar FC yenye maskani yake Turiani, Mkoani Morogoro ambayo ndiyo bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025.


Hatua hiyo inatoa ruhusa kwa mabingwa hao kushiriki Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League) katika msimu ujao wa 2025/2026 sambamba na timu Mbeya City FC kutoka jijini Mbeya ambayo imemaliza ligi hiyo ikiwa nafasi ya pili.


Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam ikipambwa na mechi ya hisani kati ya bingwa huyo na timu ya Mbeya City FC, mechi iliyoisha kwa timu hizo kutoka suluhu ya 2-2.


Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa kisiasa na serikali pamoja na viongozi mchezo huo wakiongozwa na Makamu wa pili wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Steven Mguto.


ECOBANK TANZANIA BACKS CRB 2025 ANNUAL CONSULTATIVE MEETING

Joyce Ndyetabura (left), Ecobank Tanzania Head of Commercial Banking, receives a certificate of appreciation from Minister of Works, Hon. Abdallah Hamis Ulega (MP).

Ecobank Tanzania, Dar es Salaam, 15th May 2025: Ecobank Tanzania, an affiliate of Ecobank Group, the leading pan-African banking Group, was proud to support the 2025 CRB annual consultative meeting which took place on 15th and 16th May 2025 at Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam. The chief guest was Minister of Works Hon. Abdallah Hamis Ulega (MP).


The Contractors Registration Board (CRB) was established by the Contractors Registration Act CAP R.E 2002 with a mission to regulate and develop a competitive and sustainable construction industry with capable contractors who deliver quality works and observe safety in pursuit of economic growth.


Ecobank participated in this important event as part of its commitment to support the growth and transformation of the construction and infrastructure sector in the country. As a pan-African bank with presence in over 33 countries, Ecobank brings a wealth of experience in supporting large scale infrastructure projects and SMEs through innovative digital banking products, trade finance solutions and capacity building initiatives.


We recognize the vital role contractors play in driving national development and this is a great opportunity for the Bank to be able to reach out to many contractors and offer the right solutions for their businesses. We are committed to working hand in hand with industry players by offering tailored financial solutions that address the unique needs of contractors”, said Joyce Ndyetabura, Head of Commercial Banking.

More than 1,200 participants attended the meeting.




SBL KWA KUSHIRIKIANA NA NCT WAADHIMISHA MAHAFALI YA KWANZA YA UKARIMU KWA VIJANA


Dar es Salaam, Mei 16, 2025: Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), wamefanya mahafali ya kwanza ya programu ya mafunzo ya ukarimu kwa vijana chini ya mpango wa SBL wa "Learning for Life", wenye lengo la kuwajengea vijana wa Kitanzania ujuzi wa vitendo katika sekta ya ukarimu na utalii.


Mahafali haya, yaliyofanyika katika kampasi ya NCT jijini Dar es Salaam, yalikutanisha wanafunzi 109 waliohitimu, wadau wa sekta ya ukarimu, pamoja na viongozi wa serikali. Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Mhe. Edward Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, huku Mgeni Maalum akiwa ni Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii.


Mpango huu ulioanza Septemba mwaka jana ni sehemu ya mkakati mpana wa SBL wa Society 2030: Spirit of Progress, ukilenga kuwawezesha vijana kupitia mafunzo ya vitendo, masomo darasani na mafunzo kwa vitendo kazini ili wawe tayari kuajiriwa kwenye soko la ajira linalokua la utalii na ukarimu.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Pindi Chana alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya taifa kupitia utalii shirikishi:


Utalii siyo tu kusafiri – ni injini ya ukuaji wa uchumi jumuishi, ajira kwa vijana na kubadilishana tamaduni. Tanzania inalenga kufikia watalii milioni 5 kwa mwaka, na programu kama hizi zinahakikisha tunajenga rasilimali watu sahihi kufanikisha lengo hilo.”


Alibainisha kuwa serikali imeanzisha vifurushi vipya vya vivutio vya utalii, vikiwemo utalii wa chakula, ili kutangaza utajiri wa vyakula vya asili vya Tanzania:


Watalii wa leo wanatafuta uzoefu wa kweli. Sasa tunawaletea vyakula vya asili vya Kitanzania – ‘vyakula vya asili’ – kama sehemu ya vivutio vya utalii. Kutoka kwenye chakula safi, kisicho na kemikali moja kwa moja kutoka shambani, hadi vyakula vya kipekee vya mikoa mbalimbali, utalii wa chakula utawawezesha watalii kujifunza utamaduni wetu huku pia tukikuza uchumi wa jamii zetu,” alisema Waziri.


Aidha, Dkt. Chana alisisitiza kuwa utalii ni lazima uwe endelevu, shirikishi, na wenye manufaa kwa jamii, huku akipongeza ushirikiano kati ya SBL na NCT:


Ushirikiano huu ni mfano wa ubunifu tunaouhitaji – ambapo vijana wanapewa ujuzi siyo tu wa ajira, bali wa kujenga taaluma endelevu zinazoweka mbele maadili, utamaduni na huduma bora kwa watalii wetu.”


Mhe. Edward Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, naye aliipongeza programu hiyo kwa kuchangia katika jitihada za serikali kukuza sekta ya utalii “Sekta ya utalii na ukarimu nchini Tanzania ina fursa kubwa ya kuzalisha ajira na kuchochea maendeleo ya taifa. Programu kama hii siyo tu kwamba inawapatia vijana wetu ujuzi, bali pia inasaidia kutekeleza dira ya serikali ya kugeuza utalii kuwa nguzo ya maendeleo jumuishi na endelevu. Nawapongeza SBL na NCT kwa dhamira yao ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kwa vitendo.”


Thursday, 15 May 2025

CRDB YAWAALIKA WANAHISA – MKUTANO MKUU WA 30 WA WANAHISA WAJA KWA KISHINDO!


Arusha, 14 Mei 2025: Benki ya CRDB imewataka wanahisa wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha, ambapo Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya Mwaka 2024, inayoonyesha maendeleo makubwa ya kifedha, kiutendaji na kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.



Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kwani utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa na umma, itakayofanyika Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025, katika ukumbi wa Simba, AICC. “Semina hii ya kihistoria itakuwa chini ya kaulimbiu yetu ya mwaka huu: ‘Miaka 30 ya Ukuaji wa Pamoja,’ na itafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio yetu ya pamoja, changamoto tulizozishinda, na mwelekeo wetu wa miaka ijayo,” amesema Dkt. Laay.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, kujadili mapendekezo ya maboresho ya Katiba ya Benki, kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2024 ambapo pendekezo la gawio la Sh 65 kwa hisa litawasilishwa.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa yamekamilika kwa asilimia 100. Nsekela amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki moja kwa moja na kwa njia ya kidijitali. “Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” amesema Nsekela huku akiwahakikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.



Nsekela amewahamasisha wanahisa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu huo wa kihistoria, akisisitiza kuwa uwepo wao ni muhimu kwa ajili ya kushuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 30. “Tumejenga taasisi imara inayotoa huduma bora, tumeongeza thamani kwa wanahisa, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu. Hii ni fursa adhimu kwa kila mwanahisa kujivunia sehemu yake katika mafanikio haya na kushiriki kuamua mustakabali wa benki yetu katika miaka ijayo,” amesisistiza.



Wednesday, 14 May 2025

TANZANIA HOSTS FIRST-EVER CUSTOMER EXPERIENCE CONFERENCE TO ADVANCE ECONOMIC AGENDA

Managing Director of Real Interactiv Inc. - Caroline Maajabu Mbaga, speaks to participants at the conference.

Historic gathering positions customer experience as key driver for Tanzania's economic transformation

Dar es Salaam, May 10, 2025: The inaugural Annual Customer Experience Conference, hosted by Real Interactiv Inc. in partnership with CX Academy Africa, successfully convened on May 9, 2025 at Hyatt Regency Hotel, sparking a transformative national conversation about customer experience as Tanzania's next economic frontier. The landmark event brought together more than 100 C-suite executives and public sector leaders from Tanzania's most influential organizations, including Vodacom, CRDB Bank, NBC Bank, Equity Bank, KCB, TANESCO, Helios, Strategis Insurance, Bumaco Insurance, Engie Mobisol, ZIC Takful and NSSF, to establish customer-centric strategies as fundamental to national growth.


The conference opened with powerful keynote addresses from globally recognized CX pioneers. Mandisa Makubalo, Founder and CEO of South Africa's Unlimited Experiences Group, captivated attendees with her presentation "The Voice of the Voiceless Customer," demonstrating how authentic customer understanding drives market leadership across African economies. Her insights were complemented by Jonathan Daniels, Managing Director of UK-based CX Centric, who delivered a compelling analysis of global customer-centricity trends and their specific applications for Tanzanian businesses seeking competitive advantage.


A conference highlight was CRDB Bank, Yolanda Uriyo, Head of Customer Experience as one of the sponsors, delivery of an inspiring keynote address titled "Customer Experience as Tanzania's Engine for Growth and Differentiation." With compelling examples from CRDB's transformation journey, Uriyo galvanized the audience by demonstrating how customer-centric strategies had directly contributed to the bank's market leadership and financial performance. "In today's competitive landscape, customer experience isn't just about satisfaction - it's our most powerful engine for sustainable growth and meaningful differentiation," Uriyo declared.


A pivotal moment occurred during the fireside chat "Customer Experience as a National Economic Catalyst," moderated by Caroline Maajabu Mbaga, Managing Director of Real Interactiv Inc. The discussion featured Tanzania Tourist Board Director General Ephraim Mafuru, who articulated how exceptional visitor experiences directly contribute to Tanzania's tourism sector, which accounts for nearly one-fifth of the nation's GDP. "Every interaction - from airport arrivals to hotel stays - represents either an opportunity to enhance Tanzania's global reputation or a risk to our economic potential," Mafuru emphasized. His perspective was reinforced by Felix John, Investment Promotion Manager at Tanzania Investment Center, who presented compelling data showing that investor decisions increasingly prioritize service quality alongside traditional economic factors.


The conference's practical sessions saw Tanzanian business leaders share real-world implementations of CX excellence. Vodacom's Customer Experience Operations Director Harriete Lwakatare and G4S Tanzania General Manager Imelda Lutebinga led an engaging panel on embedding customer-centric cultures within large organizations, while Dorothy Ndazi, Partner at Hilton Law Group, provided crucial guidance on balancing personalized experiences with data protection requirements.


David Makoha, Country Manager for IPSOS Tanzania, grounded the discussions in empirical evidence, presenting research demonstrating that Tanzanian companies with mature CX programs outperform sector averages by significant margins. These insights were put into practice during interactive workshops where cross-industry teams collaborated on customer journey mapping exercises under the guidance of international experts.


As the conference concluded, organizers announced several strategic initiatives to maintain momentum, including the establishment of annual Tanzania CX Innovation Awards and quarterly leadership roundtables. A complimentary resource toolkit, "50 Practical Ways to Elevate Customer Experience," was released to all attendees and made available for public download.

Tuesday, 13 May 2025

VODACOM YAZINDUA MSIMU WA 4 WA DIGITAL ACCELERATOR: BIASHARA 15 ZA KIBUNIFU KUCHUANA

Vinara 15 wa Vodacom Digital Accelerator Season 4 Watangazwa! Washindi wa msimu wa 4 wa bunifu za kampuni changa (Startups), inayoandaliwa na Vodacom Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya kampuni hiyo baada ya kutangazwa katika tukio lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  • Kufundishwa ujasiriamali na Wataalamu wa Kimataifa kutoka Marekani
Dar es Salaam, Mei 9, 2025: Vodacom Tanzania PLC, kwa kushirikiana na Huawei Tanzania, imezindua rasmi Msimu wa 4 wa Vodacom Digital Accelerator (VDA), hatua nyingine katika kusaidia ubunifu na ujasiriamali nchini.

Mwaka huu, biashara bunifu 15 zimechaguliwa kushiriki katika programu ya siku 5 ya Design Sprint, itakayoendeshwa na wataalam wa kimataifa kutoka programu ya MassChallenge ya nchini Marekani.

Lengo la Design Sprint ni kuboresha biashara zinazochipukia, kuimarisha ufanisi wa bidhaa sokoni na kuongeza maandalizi yao kwa ajili ya kuvutia uwekezaji. Kati ya hizi, biashara 10 zenye uwezo mkubwa wa kufanikiwa zitachaguliwa kwa safari ya miezi 3 ya kuendelezwa, ambapo zitapata ushauri wa kitaalam, msaada wa maendeleo ya biashara, na fursa mahususi za kufikia masoko ya ndani na ya kimataifa.


Msimu wa 4 wa VDA unaendeshwa kupitia ushirikiano wa kimkakati unaoendelea kati ya Vodacom na Huawei, jambo litakalowezesha wabunifu hao kushiriki kwenye safari ya kujifunza nchini China mwezi Juni. Wakati wa ziara hiyo ya kimataifa, wabunifu hao watakutanishwa na kampuni kubwa za teknolojia za nchini China, ili kujifunza mifumo ya ubunifu wa kisasa na pia kuwasilisha bunifu zao mbele ya wawekezaji binafsi na mashirika.

Katika hatua kubwa ya kuwaendeleza wajasiriamali chipukizi, msimu huu utakuwa na uwekezaji wa fedha taslimu zitatolewa kwa biashara tatu bora, ili kusaidia kukuza bunifu zao na hivyo kuwaongezea uwezo wa ushindani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

"VDA ni jukwaa la ukuzaji wa kizazi kijacho cha wavumbuzi wa Kitanzania. Na kwa mara nyingine tunachanganya ubunifu wa ndani na uzoefu wa kimataifa tukiwasaidia vijana wabunifu katika kujenga biashara zinazoweza kupanuka, kupata uwekezaji na kuingia kwenye majukwaa ya kimataifa," alisema Zuweina Farah, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.

Monday, 12 May 2025

STANBIC YAIMARISHA "PRIVATE BANKING" KWA WATEJA WA ARUSHA

  • Benki ya Stanbic yazindua huduma za Private Banking jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa upanuzi wa huduma zake nje ya Dar es Salaam, baada ya mafanikio ya matukio kama haya Mwanza na Mbeya mapema mwaka huu.
  • Upanuzi huu wa Arusha unaonesha dhamira ya Benki ya Stanbic kuwasogezea wateja wake huduma za kifedha za hali ya juu, na kuwapa fursa wajasiriamali, wataalamu na familia za wafanyabiashara nje ya Dar es Salaam kunufaika na Private Banking.
  • Tukio hili limeangazia kaulimbiu ya Stanbic ya “Ujasiriamali Hauishi”, likilenga kuwawezesha wateja kwa mipango ya kifedha ya muda mrefu, huduma mahususi za Private Banking, na njia za kujenga urithi wa kifamilia wa kifedha.
Arusha, 8 Mei 2025 – Benki ya Stanbic imezindua maboresho ya huduma zake za wateja maalum rasmi huduma ya Private Banking Client Value Proposition (CVP) jijini Arusha, ikionyesha dhamira yake ya kuwawezesha Watanzania wenye ukwasi mkubwa kwa kuwapatia suluhisho bora za kifedha za kiwango cha kimataifa. Uzinduzi huu unafuatia mafanikio ya matukio kama haya yaliyofanyika Mwanza na Mbeya mapema mwaka huu, na kuonyesha mkakati wa benki wa kupeleka huduma bora za kifedha nje ya Dar es Salaam.


Kupitia huduma hii, wakazi wa Arusha wananufaika kwa kuunganishwa na suluhisho za kifedha zinazowiana na mahitaji ya kipekee ya mkoa huu. Kwa kuwa Arusha ni kitovu cha biashara ya utalii, biashara ya madini, kilimo cha mazao ya biashara , na biashara za kifamilia, Private Banking inaleta thamani halisi kwa watu wanaojenga urithi wa kifamilia kupitia kazi zao za kila siku.


Arusha imechaguliwa kwa ajili ya tukio hili muhimu kutokana na umuhimu wake wa kiuchumi na kijamii. Kama kitovu cha utalii, diplomasia, kilimo, na biashara zinazokua kwa kasi, Arusha ina jamii yenye nguvu ya viongozi wa biashara, wawekezaji na wataalamu wanaotafuta huduma za kifedha za kiwango cha juu. Pia ni lango kuu la Afrika Mashariki na makao ya taasisi nyingi za kimataifa, hivyo kuifanya kuwa soko muhimu kwa huduma za Private Banking.

Tukio la Arusha limewakutanisha wateja maalum wa Benki wa Private Banking, wajasiriamali na wadau wakuu kujadili jinsi huduma hizi zinavyoweza kusaidia kukuza, kusimamia, na kulinda utajiri wa kifamilia kwa vizazi vijavyo. Kwa kauli mbiu ya 'Ujasiriamali Hauishi,' tukio hili limeangazia umuhimu wa mipango ya kifedha ya muda mrefu, urithi wa kifedha, na huduma za kipekee zinazolenga tabaka la juu la Tanzania.

Arnold Shirima, mtoa huduma za utalii kutoka Usa River, alishiriki uzoefu wake;

Huduma hii imenisaidia kupanga kwa mikakati zaidi kuhusu mustakabali wa biashara yangu. Kama mtu anayesimamia mapato ya msimu, nafasi nyingi za kuhudumia wateja, na gharama kubwa za uendeshaji, nimejifunza jinsi ya kutenganisha fedha za binafsi na za biashara bila kuathiri ubora wa huduma au ukuaji wa biashara. Kupitia msaada wa Benki ya Stanbic, sasa najisikia kuwa na udhibiti zaidi wa fedha zangu na nina uwezo bora wa kukuza biashara kwa njia endelevu". Arnold Shirima, mkulima wa mazao ya biashara katika maeneo ya Usa River, anasema: “Huduma hii imenisaidia kupanga mikakati ya kifedha ya muda mrefu. Kwa sasa ninafahamu namna ya kutenganisha fedha za biashara na matumizi binafsi bila kuathiri ukuaji wa shamba langu.”

STANBIC YAZINDUA KAMPENI YA “SALARY SWITCH” KWA ZAWADI NA MANUFAA MAALUM


  • Benki ya Stanbic Tanzania yazindua kampeni mpya ya Salary Switch, inayotoa zawadi za kila siku za pesa taslimu na mikopo ya mshahara kwa wafanyakazi waliopata ajira rasmi.
  • Kampeni inalenga kuimarisha uthabiti wa kifedha wa muda mrefu kwa kuhamasisha kuweka akiba kwenye akaunti za watoto, na kukuza utamaduni wa kuokoa.
  • Droo za bahati nasibu zinatoa fursa kwa wafanyakazi kote Tanzania kujishindia zawadi kubwa za pesa kwa urahisi kwa kutumia huduma za Stanbic Bank.
Dar es Salaam: Benki ya Stanbic Tanzania imezindua rasmi kampeni mpya ya Salary Switch, inayolenga kuwazawadia Watanzania waliopo kwenye ajira rasmi kwa zawadi za kila siku za pesa taslimu, mikopo ya mshahara ya kidigitali, na upatikanaji rahisi wa mikopo hadi TZS milioni 150. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itaanza tarehe 1 Mei hadi 30 Julai 2025, na inalenga wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma, kuwapatia urahisi wa kifedha wa haraka, motisha, na huduma bora za kidigitali.

Kupitia kampeni hii, wateja watakaohamishia mishahara yao Stanbic Bank wataweza kushiriki kwenye droo za bahati nasibu za kila siku (Jumatatu hadi Ijumaa), zenye zawadi za pesa taslimu zinazotofautiana kati ya TZS 100,000 hadi TZS 500,000 kulingana na siku.

Zaidi ya hayo, wateja wanaofungua Akaunti ya Akiba ya Mtoto (Hatua) watazawadiwa na benki kwa kulinganisha kiasi cha awali kilichowekwa hadi TZS 250,000, ili kuwapa watoto wao mwanzo mzuri wa kifedha. Kwa wateja waliofungua akaunti hiyo tayari, kuweka amri ya kudumu ya kujiwekea akiba pia kutaleta zawadi kama hiyo – benki italinganisha kiasi kinachowekwa hadi TZS 250,000.

VISA APPOINTS NEW COUNTRY MANAGER FOR TANZANIA, UGANDA, BURUNDI AND RWANDA


12th May 2025, Dar es Salam – Visa, a world leader in digital payments, has appointed Victor Makere as the new Country Manager for Tanzania, Uganda, Burundi and Rwanda. Victor will be responsible for driving Visa’s strategic growth, enhancing client relationships, and expanding digital payment solutions across these key markets.

Victor will manage a diverse client portfolio across the four countries, aiming to boost Visa's strategic value, increase revenue for both clients and Visa, and strengthen executive relationships. He will also set business objectives and lead key projects, including new product and service implementation.

Chad Pollock, Vice President and General Manager for East Africa at Visa, commented on the appointment: “We are delighted to welcome Victor to the Visa East Africa leadership team. With his distinguished track record in digital financial services, merchant acquiring, and strategic business development, we look forward to his significant contributions to Visa’s efforts to enhance financial inclusion and expand digital commerce across Tanzania, Uganda, Burundi, and Rwanda. His leadership and expertise will be invaluable as we continue to build a resilient and inclusive digital payments ecosystem in the region.”

Victor expressed his enthusiasm for the new role: “I am excited to join Visa and play a key role in accelerating the growth of digital payments across Tanzania, Uganda, Burundi, and Rwanda. Visa’s commitment to financial innovation and inclusion aligns perfectly with my vision for transforming the payments landscape. I look forward to collaborating with our clients, partners, and stakeholders to deliver cutting-edge, secure, and seamless payment solutions that drive economic growth and empower businesses and consumers across the region.”