- Kufundishwa ujasiriamali na Wataalamu wa Kimataifa kutoka Marekani
Mwaka huu, biashara bunifu 15 zimechaguliwa kushiriki katika programu ya siku 5 ya Design Sprint, itakayoendeshwa na wataalam wa kimataifa kutoka programu ya MassChallenge ya nchini Marekani.
Lengo la Design Sprint ni kuboresha biashara zinazochipukia, kuimarisha ufanisi wa bidhaa sokoni na kuongeza maandalizi yao kwa ajili ya kuvutia uwekezaji. Kati ya hizi, biashara 10 zenye uwezo mkubwa wa kufanikiwa zitachaguliwa kwa safari ya miezi 3 ya kuendelezwa, ambapo zitapata ushauri wa kitaalam, msaada wa maendeleo ya biashara, na fursa mahususi za kufikia masoko ya ndani na ya kimataifa.
Katika hatua kubwa ya kuwaendeleza wajasiriamali chipukizi, msimu huu utakuwa na uwekezaji wa fedha taslimu zitatolewa kwa biashara tatu bora, ili kusaidia kukuza bunifu zao na hivyo kuwaongezea uwezo wa ushindani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
"VDA ni jukwaa la ukuzaji wa kizazi kijacho cha wavumbuzi wa Kitanzania. Na kwa mara nyingine tunachanganya ubunifu wa ndani na uzoefu wa kimataifa tukiwasaidia vijana wabunifu katika kujenga biashara zinazoweza kupanuka, kupata uwekezaji na kuingia kwenye majukwaa ya kimataifa," alisema Zuweina Farah, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.
Tangu kuanzishwa kwake, Vodacom Digital Accelerator imewezesha zaidi ya biashara chipukizi 75 nchini kwa kuwapatia nyenzo, mtaji na kuwakutanisha na wajasiriamali na makampuni makubwa iliyowawezesha kukua na kustawi. Msimu wa 4 unaendeleza urithi huu, kwa dhamira mpya ya ujumuishwaji wa kidijitali, uhifadhi wa baiyoanuai, ujasiriamali wa vijana na uwezeshaji wa kiuchumi.
Kuhusu Vodacom Digital Accelerator (VDA):
Vodacom Digital Accelerator (VDA) ni programu Iliyoanzishwa mwaka 2019 na Vodacom tanzania PLC kwa lengo kuu ya kusaidia biashara chipukizi za kiteknolojia kukua. VDA hutambua, kulea, na kukuza biashara changa na zinazokua za kiteknolojia zenye lengo la kutatua changamoto za jamii kwa njia ya ubunifu. Programu hii inachanganya ushauri wa kitaalam, ufikiaji wa masoko, maandalizi ya uwekezaji, na uzoefu wa kimataifa ili kusaidia biashara chipukizi za Kitanzania kustawi katika uchumi wa kidijitali unaoshindana.
No comments:
Post a Comment