Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) akiwapongeza wachezaji wa timu ya Mbeya City wakati wa hafla hiyo. |
Kwa upande wake Masuke alisema benki hiyo inayodhamini ligi tatu muhimu hapa nchini kwa udhamini wenye thamani ya shilingi bilioni 32 itaendelea kuboresha zaidi ligi hizo ili ziendelee kutoa matokeo chanya kitaifa na kimataifa kulingana na malengo ya udhamini huo ikiwemo suala zima la kuzalisha ajira ambapo kwa sasa zaidi ya ajira 7,000 za moja kwa moja zimezalishwa kupitia udhamini huo.
“Tunawapongeza sana washiriki wote wa ligi ya Championship lakini kiupekee zaidi tunawapongeza Mtibwa Sugar FC kwa kuibuka washindi kwenye ligi hii. Pongezi zetu pia tunazielekeza kwa Mbeya City FC kwa kuwa mshindi wa pili na hivyo nae pia anakwenda kushiriki Ligi kuu ya NBC msimu ujao…hongereni sana,’’ alisema Masuke .
Kwa mujibu wa Bw Masuke benki hiyo inajivunia sana mafanikio ya vilabu vinavyofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushindani bora uliopo kwenye ligi za ndani.
“Kwetu mafanikio hayo ni kama motisha ya kuedeleza zaidi jitihada za kuioboresha zaidi ligi hizi zote tatu kupitia udhamini na utoaji wa huduma za kifedha mahususi kwa wadau wake ikiwemo mikopo ya vyombo vya usafiri kwa vilabu, bima za afya kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi pamoja utoaji wwa elimu ya fedha kwa wachezaji na vilabu shiriki.
Akizungumzia ubingwa huo Nahodha wa Mtibwa Sugar FC, Oscar Masai pamoja na kuwashukuru wadau wote kwa jitihada zao zilizosaidia kufanikisha ubingwa huo akiwemo mdhamini huyo kwa kuandaa mazingira mazuri kwa timu zote shiriki, aliahidi kwa niaba ya wachezaji wenzake kuhakikisha wanajipanga vema ili waweze kutoa ushindani zaidi kwenye ligi kuu ya NBC msimu ujao.

No comments:
Post a Comment