![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akionyeshwa mabenchi ya kukalia katika Hospitali ya Kigamboni na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard yaliyotolewa msaada na Benki hiyo. |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akionyeshwa madawati na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Msingi Ungindoni. |
Benki ya NMB, imekabidhi misaada yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 25 kwa Shule tatu za Msingi, moja ya Sekondari na Hospitali ya wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, pamoja na a Wilaya hiyo, iliyotolewa kupitia mwamvuli wa Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatuma Almasi Nyangasa katika hafla iliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni na Shule ya Msingi Ungindoni.
Shule za Msingi zilizonufaika ni Ungindoni (madawati 50 yenye thamani ya Sh. Mil. 5), Raha Leo (mabati 200 Sh. Mil. 6.4), Kigamboni Sekondari (mabati 180 Sh. Mil. 5.7) na Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni (mabenchi 20 ya kukalia wagonjwa wakati wakisubiri matibabu, Sh. Mil. 8).
Akizungumza katika hafla hiyo, Donatus aliushukuru uongozi wa shule hizo na hospitali hiyo 0kwa kuitambua NMB Kama mshirika sahihi na wa uhakika wa changamoto za elimu na afya, kiasi cha kupeleka maombi yao kwa benki hiyo.





























