Washindi kutoka Timu za NMB, wakiwa na medali zao walizoshinda katika michezo mbalimbali. |
Timu ya Mpira wa miguu ya NMB ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NMB - Dk. Edwin Mhede wakiwa tayari kwa michuano na timu ya Bunge Sports Club. |
Wanaume kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kazi, Philbert Casmir wakipambana katika mchezo wa kuvuta Kamba dhidi ya wenzao kutoka Bunge Sports Club. |
Timu ya wanawake ya NMB na Bunge Sports Club wakichuana katika mpira wa Pete. |
Timu ya Mpira wa Kikapu kutokaa NMB na Bunge Sports Club wakichuana. |
Afisa Mkuu wa Rasilimaliwatu wa NMB, Emmanuel Akonaay, akitetea timu yake ya Mpira wa miguu dhidi ya Bunge Sports Club katika mchezo uliochezwa katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. |
Iilikuwa ni zaidi ya Kivumbi na Jasho, kuanzia katika matembezi ya taratibu yaliyoongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Phillip Isdor Mpango, hadi kwenye michezo saba iliyoshondaniwa, Kivumbi kikitimka zaidi katika mpira wa miguu na kikapu, ambako vuta nikuvute ilikuwa kubwa.
Katika mpira wa miguu, Bunge FC ilitoshana nguvu na NMB kwa dakika 90 ndani ya dimba la Jamhuri, ndipo Sheria ya upigaji penalti ulipotumika kumsaka bingwa, ambako Bunge FC waliibuka kidedea wakifunga penalti 4-3 katika mikwaju sita sita waliyopigiana.
Mnyukano kama huo ulikuwepo katika kikapu, ambako licha ya kutawala mechi na 'kuupiga mwingi,' NMB ilijikuta ikipoteza mchezo kwa kufungwa vikapu 70-57, hasira za kupoteza mchezo huo zikawapeleka katika riadha kwa hasira na kutawala mbio za mita 100 na 400 wanawake na wanaume.
Teddy George wa NMB akatwaa medali mbili za dhahabu mita 100 na 400 kwa wanawake akiwabwaga Rose Tweve na Queen Mlay wa Bunge, huku Nsolo Mlozi wa NMB naye akimgaragaza Aboubakar Assenga wa Bunge katika mita 100 wanaume, na kwenye mita 400 wanaume, Mlozi akitwaa medali akifuatiwa na Juma Kimori wa NMB pia.
Ushindi pekee wa Bunge katika mbio ni aliopata Naibu Spika, Tulia Ackson, aliyeshinda Mita 100 Menejimenti, akimshinda Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna aliyeshika nafasi ya pili akifuatiwa na Janeth Shango wa NMB pia katika nafasi ya tatu.
Katika mbio za kukimbiza kuku, NMB iliibuka mabingwa upande wa wanawake na wanaume, ingawa ilifanya vibaya katika kuvuta kamba na wavu (wanawake na wanaume), ambako Bunge Sports Club ilishinda.
No comments:
Post a Comment