Michezo hiyo itafanyika baina ya Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa Benki ya NMB ikiwa pia ni maandalizi ya mbio za NMB Marathon 2021- Mwendo wa Upendo zitakazo fanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18 Septemba 2021.
Tamasha la 'Kivumbi na Jasho', linatarajia kufanyika Jumamosi Septemba 4, 2021 kwenye viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema licha ya kutumika kujenga mahusiano mema baina ya taaisi hizo, tamasha hilo ni sehemu ya juhudi za Benki ya NMB kuhakikisha jamii ya Kitanzania inapenda michezo, ambayo ni muhimu kwa afya na pia ni ajira.
Alisema wanajisikia furaha kupata nafasi adhimu ya kujumuika pamoja na watunga Sheria hao, ambao Wengi wao ni wateja wao, hivyo wanaushukuru uongozi wa Bunge na Kamati ya Utendaji ya Bunge Sports kwa kukubali kutenga muda wa kushiriki Tamasha hilo.
Mponzi alieleza mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Sports, Tarimba Abbas ambaye ni Mbunge wa Kinondoni kuwa
watalianza Tamasha la Kivumbi na Jasho kwa mbio za taratibu 'jogging' asubuhi kuanzia viwanja vya Bunge hadi Chinangali Park, kisha michezo mingine ikiwamo kuvuta kamba, kikapu, netiboli, wavu, kukimbiza kuku na mpira wa miguu kisha kukabidhi zawadi washindi.
Akitoa neno la shukrani, Tarimba aliipongeza NMB kwa dhamira ya dhati ya kuimarisha mahusiano baina ya taasisi hizo kiasi cha kuwaandalia tamasha hilo na kwamba Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesisitiza na kuonesha umuhimu na thamani ya Kivumbi na Jasho, na wao kama wabunge wapo tayari kukiamsha jumapili ili na wao wawe sehemu ya Mwendo wa upendo upendo unaolenga kurejesha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya Fistula kwani wanaamini Fistula inatibika.
No comments:
Post a Comment