Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926

Absa Banner_170926

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Friday, 9 October 2020

BENKI YA I&M YASHEHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano Oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.

Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano Oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.
Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano Oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.
Wafanyakazi wakiwa pamoja na wateja wa benki ya I&M siku ya Jumaatano ambapo benki hiyo iliadhimisha kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata keki na wateja wao waliotembelea benki siku hiyo. Licha ya kukata keki pia benki ilichukua fursa ya kutembelea wateja wa kila ngazi, kutoa zawadi kama shukrani kwa wateja pamoja na kuvaa mavazi ya aina mbalimbali kuonyesha utofauti na furaha ya kuhudumia.
Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakitoa zawadi kwa mteja wa benki hiyo kama moja ya njia ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuitumia na kuiamini Benki ya I&M kwa huduma bora inazotoa kwa wateja wake na jamii kwa ujumla.
Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano Oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.
Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiwa katika mavazi ya udaktari wakionyesha kuwapatia wateja suluhisho la changamoto za kifedha kwa kuwapatia wateja huduma bora kibenki ili kufanikisha shughuli za kibiashara na uchumi. Haya yote yamefanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiwa katika mavazi ya udaktari wakionyesha kuwapatia wateja suluhisho la changamoto za kifedha kwa kuwapatia wateja huduma bora za kibenki ili kufanikisha shughuli za kibiashara na uchumi. Haya yote yamefanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mfanyakazi wa Benki ya I&M katika mavazi ya udaktari akiwa anatoa huduma kwa mmoja kati ya wateja waliotembelea tawi la benki hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Dar es Salaam - Benki ya I&M Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kutambua mchango muhimu unaotolewa na fanyakazi wake katika kuwahudumia wateja wao kwa viwango vya juu na kuhakikisha kuwa wanakuwa wenye furaha wakati wote.

Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni maktaba square jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya benki hiyo, ikiambatana na shughuli mbalimbali kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa wateja wanaothaminiwa na pia wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu muhimu la kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote.

Miongoni mwa shughuli za kusherehesha hafla hiyo na wiki ya huduma kwa wateja zilizofanywa na benki hiyo ni pamoja na Maofisa wa juu na waandamizi wa benki hiyo akiwamo Afisa Mtendaji Mkuu, walichukua jukumu la kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali kwa siku ya leo.

Sheherehe hiyo ya wiki nzima ni matokeo ya kujitolea kwa benki hiyo ya I&M katika kuongeza ushiriki wa wafanyakazi katika kuunga mkono kaulimbiu ya mwaka huu ya siku hiyo inayosema kuwa, ‘Timu ya ndoto’.

BENKI YA DCB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA IKIAHIDI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (wa nne kushoto), akikata keki kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika katika Tawi la DCB Uhuru, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano katika tawi hilo, Olen Misigaro, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo, Isidori Msaki (wa pili kulia) na baadhi ya wateja.

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (wa tatu kushoto), akikata keki kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika katika Tawi la DCB Uhuru, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendajiwa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo, Isidori Msaki (wa pili kulia) na baadhi ya wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano tawini hapo, Olen Misigaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo, Amir Amirali katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam. Anayeangalia ni mteja mwingine, Joachim Kimanza.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Zacharia Kapama (kulia), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam. Katikati ni maofisa uhusiano katika tawi hilo, Getrude Mziray (wa pili kushoto) na Olen Misigaro.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DCB, Isidori Msaki (wa pili kushoto), akisalimiana na mmoja wa wateja wa benki hiyo, Joachim Kimanza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.

Meneja Uhusiano wa Benki ya DCB wa Tawi la Uhuru, Olen Misigaro (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Rahma Ngassa (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto), akimpa keki mmoja wa benki hiyo, Theresia Lyimo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo katika Tawi la Uhuru, Kariakoo, Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Zawadia Nanyaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), Mkurugenzi wa Biashara, Zacharia Kapama na Meneja Uhusiano wa DCB Tawi la Uhuru, Olen Misigaro wakisalimiana na baadhi ya wateja tawini hapo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo, Kariakoo, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey Ndalahwa akizungumza na baadhi ya wateja katika tawi la Temeke kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Francis Kafuku (wa tatu kulia) na Meneja wa benki hiyo tawi la Temeke, Anna Kasyupa (kushoto) wakikata keki pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akizungumza na baadhi ya wateja katika tawi la Temeke kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia muda wao kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali ya benki hiyo.

TELECOM SECTOR HOLDS THE POTENTIAL TO FACILITATE THE NEXT GENERATION OF INVESTMENT AND TECHNOLOGY IN TANZANIA

It is fair to say that the evolution of technology has had a significant impact on our daily lives.

Perhaps one of the most striking areas of technological innovation is in mobile internet. In recent years, the rise of mobile internet and mobile assisted applications has become an indispensable force which has created many benefits.

For businesses, mobile internet has become a vital tool for being able to work collaboratively, even when teams and colleagues are in different cities or countries. It has also provided these businesses with a way to advertise their goods and services to markets that might have once been harder to reach.

In a similar way, mobile internet has enabled social media platforms like Facebook, Twitter or Instagram to become an essential means of staying in touch with our friends and family, simply through the click of a button.

Given this, it is not surprising that the country has a fast-growing mobile internet landscape with the overall penetration rate doubling between 2013 and 2019. It is likely to increase further in the years ahead.

NMB BANK UNVEILS PARTNERSHIP WITH UNION PAY INTERNATIONAL

Zanzibar’s Minister for Information, Tourism and Heritage, Mahmoud Thabit Kombo symbolizes cash withdrawal using a Union Pay Card at an NMB Bank ATM. Looking on are the bank’s Chief Executive Officer, Ruth Zaipuna (second left), Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi (second right) and other top officials at the bank.

Zanzibar’s Minister for Information, Tourism and Heritage, Mahmoud Thabit Kombo (second right) and top officials from NMB Bank led by the Bank’s Chief Executive Officer, Ruth Zaipuna displaying the new logo for NMB Pay.
Zanzibar’s Minister for Information, Tourism and Heritage, Mahmoud Thabit Kombo exchanges a light moment with NMB Bank’s Chief Executive Officer, Ruth Zaipuna and the Bank’s Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi.

NMB Bank Plc has announced the debut of offering services with UnionPay International that enables UnionPay cardholders worldwide to access services at NMB ATMs, merchant Point-of-Sales (POS) and e-commerce platform across Tanzania. NMB Bank merchants are also enabled to accept online payments on their websites.

The NMB Bank Chief Executive Officer, Ruth Zaipuna, said the UnionPay acquiring services being launched will facilitate quick, easy and secure payment services enabling real-time access to UnionPay cardholders to their funds with extra digital value-added services.

“This is another milestone on NMB Bank’s commitment to enhance customer service access and experience. It is also an opportunity for merchants such as retail stores, hotels, tour operators to boost their cross-border businesses by accepting online payments,” she said.

“With our chain of more than 1,750 POS terminals and over 800 ATMs across the country, the service is expected to significantly benefit UnionPay cardholders.”

Thursday, 8 October 2020

BENKI YA NMB, NHIF WAWEKA HISTORIA AFYA KWA WOTE

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF, Bernard Konga (kushoto) wakisaini mkataba wa uzinduzi wa Mpango wa DUNDULIZA kwa huduma za NHIF kupitia Benki ya NMB. Kulia ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa NHIF, Bernard Konga (kushoto) wakibadilishana mkataba wa uzinduzi wa Mpango wa DUNDULIZA kwa huduma za NHIF kupitia Benki ya NMB. Kulia ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.

Benki ya NMB na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zimeweka historia mpya na ya aina yake nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kipekee wa bima ya afya utakaowawezesha wananchi wengi kupata huduma hiyo kiurahisi na kwa nafuu kubwa kwa kuweka akiba kidogo kidogo kulingana na vipato vyao.

Historia hiyo iliandikwa jijini Dar es Salaam baada ya taasisi hizo mbili kuingia makubaliano ya kutekeleza mpango huo ambao unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwenye malengo ya taifa ya kuboresha rasilimali afya na upatikanaji wa tiba.

Mpango huo mahsusi wa huduma ya afya kwa wote ujulikanayo kwa jina la DUNDULIZA ulizinduliwa katika hafla iliyofanyika PSSSF Complex na kuhudhuriwa na viongozi na wafanyakazi wa taasisi hizo mbili pamoja na wadau mbalimbali.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna, na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga,walisema ukubwa wa mtandao wa huduma wa benki hiyo utasaidia sana kuipeleka DUNDULIZA kwa Watanzania hasa wale wa kawaida kama wakulima na wajasiliamali. Pia walisema kuwa huduma hiyo mpya itakuwa na mchango mkubwa katika mipango ya serikali ya kuhakikisha afya bora kwa Watanzania wote kupitia bima ya afya.

ABSA BANK RECOGNIZES ITS ESTEEMED CUSTOMERS

Absa Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser giving his keynote remarks at a function organized by the bank to recognize some of its long standing customers and external stakeholders being part of the bank's 2020 customer service month celebrations. A brief occasion was held in Dar es Salaam recently.
Absa Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser (centre), presenting a certificate of appreciation to one of its long-standing customer, Prudence Masaku at a function organized by the bank to recognize its long-standing customers and external stakeholders being part of the bank's 2020 customers service month celebrations in Dar es Salaam recently. Looking on is Absa Head of Corporate Client Service, Minal Sanghvi.
Absa Bank Tanzania Chief Financial Officer, Obedi Laiser (centre), presenting a certificate of appreciation to one of its long-standing customer, Julius Massawe at a function organized by the bank to recognize its long-standing customers and external stakeholders being part of the bank's 2020 customers service month celebrations in Dar es Salaam recently. Looking on is Absa Head of Retail Products & Strategy, Heristraton Genesis.
Absa Bank Tanzania Director of Compliance & Legal, Irene Sengati Giattas (centre), presenting a certificate of appreciation to one of its long-standing stakeholder, Margaret Nyangusi at a function organized by the bank to recognize its long-standing customers and external stakeholders being part of the bank's 2020 customers service month celebrations in Dar es Salaam. Looking on is ABT Chief Financial Officer, Obedi Laiser.
Some members of Absa Bank Tanzania management team pose for a souvenir photograph with the bank’s external stakeholders during the ceremony.
Some members of Absa Bank Tanzania management team pose for a memento photograph with some of the bank’s long-standing customers during the ceremony.
Today we kick off our Customer Service Month celebrations, as we honor the importance of providing our loyal and valued customers with outstanding service. This is the first time Absa Bank Tanzania celebrates and recognizes the support we get from customers since the adaption of our new name.

Along with customers, Absa Bank Tanzania also recognize our external dream team that has shown their utmost dedication and provided extraordinary services that have enabled us to serve our customers better.Indeed, the celebrations are about recognizing our longstanding customers who have been part of the story of our growth and change since 2000 when we first opened doors in Tanzania.

MAISHA MAGIC BONGO CELEBRATES MILESTONE OF 5 YEARS OF MAGIC

A platform with the most exciting content and where authentic Tanzanian stories are told…

Maisha Magic Bongo launched on the October 2015 on DSTV Channel 160. With great determination and attention to the Tanzanian language, culture and taste, the channel has since grown to be the most loved local channel amongst the homogenous target market.

Throw back to where all the magic began

“The channel was initially launched as a predominantly movie channel coupled with lifestyle shows. As audience demand grew, this inclined the platform to add local Drama’s, Telenovela’s, Lifestyle as well as Indian dubbed content which has a massive following in the market that we operate in” said Barbara Kambogi, the Head of Channel since its inception. Hands up to those who can recall Mzooka- the one-hour music show that featured the latest in urban hits from Tanzania, Talaaka- the drama series that kept you and your loved ones glued to your seats weekdays or the celebrity cooking show, Jikoni na Marion that put your cooking skills to the test as well as the riveting drama series- Kapuni and Sarafu!

A leader in the Tanzanian local entertainment space

“We work with the best producers whom we groom and mentor to produce world class content” said Kambogi. “Throughout the past 5 years, the channel has gone through a complete content overhaul whilst addressing the entertainment needs of the Tanzanian viewers and developing the entertainment industry and economy of the region.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TIGO, SIMON KARIKARI ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WATEJA WA TIGO KATIKA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari pamoja na viongozi mbalimbali wa idara wakijibu na kutatua maswali ya wateja wa Tigo katika kituo cha huduma kwa wateja namba 100, zoezi limefanyika  jana katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Bi. Mwangaza Matotola, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo, Bw. Simon Karikari pamoja na viongozi wa idara mbalimbali katika kituo cha kisasa cha Huduma kwa Wateja. Tukio hilo liliambatana na ukataji wa keki.
Mkurugenzi wa Tigo, Bw. Simon Karikari akipokea keki kutoka kwa Mwangaza Matotola, Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja kama ishara ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Tigo inawathamini na kuwajali kwa kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma na bidhaa bora zaidi kila siku.

Watoa huduma wa Tigo wakifurahia maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora wanazostahiri sehemu yeyote.


Watoa huduma wa Tigo wakifurahia maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora wanazostahiri sehemu yeyote.

Watoa huduma wa Tigo wakifurahia maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora wanazostahiri sehemu yeyote.
Watoa huduma wa Tigo wakifurahia maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora wanazostahiri sehemu yeyote.

Wednesday, 7 October 2020

BENKI YA CRDB YADHAMINI LIGI YA TAIFA YA MPIRA WA KIKAPU

Benki ya CRDB imetangaza udhamini wa shilingi milioni 200 kwa ligi ya mpira wa kikapu ya taifa 2020 itakayofanyika Dodoma katika viwanja vya Chinangali kuanzia tarehe 12 Novemba na kilele chake ni 21 Novemba, 2020. 

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema benki hiyo imefikia makubaliano na Shirikisho la Taifa la Mpira wa Kikapu (TBF) ya udhamini wa ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu ambayo imepewa jina la “CRDB Bank Taifa Cup”.

Mwambapa alisema udhamini wa ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu ni muendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo. Aliongezea kuwa Benki hiyo kupitia sera yake ya Uwezeshaji katika Jamii (CSI Policy) imekuwa ikiwekeza katika michezo ya vijana kwa kuamini kuwa inasidia kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.
Akizungumzia kuhusu msukumo uliopelekea Benki hiyo kudhamini ligi hiyo ya taifa ya kikapu yenye kauli mbiu ya “Ni Zaidi ya Game, Ni Maisha”, Mwambapa alisema mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa haupewi sana kipaumbele kulinganisha na michezo mingine, Hivyo kupelekea kiwakatisha tamaa vijana wengi ambao wamekuwa wakionyesha vipaji katika mchezo huo.

“CRDB Bank Taifa Cup” inakuja kuleta hamasa si tu kwa vijana na wapenzi wa mpira wa kikapu bali kwa Watanzania wote kwa kuwaonyesha umuhimu wa kuwekeza katika michezo ya vijana na fursa zilizopo ikiwamo ajira,” alisema Mwambapa.

Mwambapa alisema mbali na zawadi zitakazokuwa zikitolewa kwa timu zitakazofanya vizuri katika “CRDB Bank Taifa Cup”, Benki ya CRDB pia imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya “Scholarship” kwa wachezaji watakaofanya vizuri.
“Tutakuwa pia na zawadi kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa kikapu katika kila hatua za mashindano. Niwaombe watanzania waanze kutufuatilia kupitia Azam TV na mitandao yetu ya kijamii kujua namna ya kushiriki,” aliongezea Mwambapa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mike Mwita aliishukuru Benki ya CRDB kwa kudhamini ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu huku akisema udhamini huo utaongeza mapenzi ya mpira wa kikapu kwa vijana kama ilivyo kwa mpira wa miguu na michezo mingine.

Mwita alisema: "Tunafurahi sana kwa udhamini na ushiriki thabiti wa Benki ya CRDB katika jitihada hizi zinazolenga kukuzwa kwa mpira wa kikapu nchini. Sio tu kwamba udhamini wa Benki ya CRDB utaboresha kiwango cha ligi, lakini pia utavutia Watanzania wengi kufuatilia mchezo huu na kuhamasisha vijana wengi kushiriki."
Naye Msimamizi wa vipindi vya michezo Azam TV, Michael Maluwe amewataka Watanzania kuanza kufuatilia CRDB Bank Taifa Cup kupitia chaneli ya michezo ya Azam Sports 2, ambapo Benki hiyo imeanzisha kipindi maalum kuelekea mashindano hayo ya mpira wa kikapu. “Azam TV itaweka kambi Dodoma kuwaletea burudani Watanzania kuelekea mashindano haya, niwakaribishe Watanzania tujiunge na Azam TV ili kuwashangilia vijana wetu,” alisema Maluwe.

CRDB Bank Taifa Cup inatarajiwa kuhusisha timu 36 za mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume na wanawake. Mashindano hayo pia yatatanguliwa na michuano ya timu za veteran zza Benki ya CRDB, Bunge, Pazi, Bahari na timu za walemevu. Pamoja na Benki ya CRDB kuwa mdhamini mkuu, CRDB Bank Taifa Cup pia imedhaminiwa na Azam TV, kampuni ya bima ya Sanlam na kampuni ya maji ya Cool Blue.