Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_301026_111126

Stanbic Bank Banner_201026

Sunday, 22 November 2026

BENKI YA EXIM TANZANIA YALINDA HUSTLE ZA MADEREVA KUPITIA TWENDE BBM FESTIVAL 2026

Yawasogezea madereva wa bodaboda, bajaji na magari huduma za malipo ya kidijitali, bima na huduma za kibenki zinazolenga kulinda vyanzo vyao vya kipato.

Dar es Salaam, 14 Novemba 2026: Benki ya Exim Tanzania imetumia tamasha la Twende BBM Festival 2026 kuwasogezea madereva wa bodaboda, bajaji na magari huduma za kifedha zinazolenga kurahisisha shughuli zao za kila siku na kulinda vyanzo vyao vya kipato, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wake na wadau wa sekta ya usafiri nchini.

Ikiwa mdhamini wa tamasha hilo, Benki ya Exim ilitumia fursa hiyo kuwafikia madereva wanaohusishwa na jukwaa la Twende. Jukwaa hilo linahusisha madereva takribani 12,000 na jumuiya pana ya zaidi ya watumiaji 46,000 wa huduma zake. Kupitia tamasha hilo, Benki ya Exim ilipata fursa ya kukutana na madereva na kuwafahamisha kuhusu huduma za kifedha zinazoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.

Katika tamasha hilo, Benki ya Exim iliendeleza ujumbe wa kampeni ya “Exim Inalinda Hustle Yako” kwa kutambulisha huduma nne zinazolenga kukidhi mahitaji ya madereva katika shughuli zao za kila siku. Huduma hizo ni Exim Lipa ChapChap, Tumaini Health Insurance, Motor Insurance na Exim Quick Account. Kwa pamoja, huduma hizi zinalenga kurahisisha upokeaji wa malipo, kuwawezesha madereva kupata ulinzi wa afya na kulinda vyombo vya usafiri wanavyotegemea kujipatia kipato.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi katika Benki ya Exim Tanzania, alisema kuwa benki inatambua mchango wa madereva katika kurahisisha huduma za usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi. Hivyo, inaendelea kuwasogezea huduma zinazowasaidia kusimamia shughuli zao na kulinda vipato vyao.

“Kwa madereva wengi, bodaboda, bajaji na magari si vyombo vya usafiri pekee, bali ni nyenzo muhimu za kujipatia kipato na kutunza familia zao. Tunatambua changamoto na mahitaji yanayoambatana na kazi zao za kila siku. Ndiyo maana, kupitia huduma zetu, tunalenga kurahisisha upatikanaji wa malipo, kuwapatia fursa ya kupata ulinzi wa afya na vyombo vyao vya usafiri, pamoja na huduma za kibenki zinazowawezesha kusimamia fedha zao kwa urahisi zaidi. Hii ndiyo maana halisi ya ujumbe wetu, Exim Inalinda Hustle Yako,” alisema Lyimo.

Kupitia Exim Lipa ChapChap, madereva wanaweza kurahisisha upokeaji na ufanyaji wa malipo. Tumaini Health Insurance inawawezesha kupata ulinzi wa bima ya afya, huku Motor Insurance ikitoa ulinzi wa bima kwa vyombo vya usafiri wanavyotumia katika shughuli zao za kila siku. Kwa upande mwingine, Exim Quick Account inawapa fursa ya kufungua akaunti na kupata huduma za kibenki za Exim.

Mmoja wa madereva walioshiriki tamasha hilo, alisema kuwa ushiriki wa Benki ya Exim umewapa madereva fursa ya kufahamu huduma za kifedha zinazoweza kuwasaidia kusimamia na kulinda shughuli zao za kila siku.

“Ni jambo zuri kuona taasisi za kifedha zikija karibu nasi na kutuletea huduma zinazozingatia mahitaji yetu. Kazi yetu ya kila siku inategemea vyombo vyetu vya usafiri na uwezo wetu wa kuendelea kufanya kazi ili kupata kipato. Kwa hiyo, kufahamu huduma za malipo na bima zinazoweza kutusaidia kulinda kazi zetu ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwetu,” alisema.

Kupitia ushiriki wake katika Twende BBM Festival 2026, Benki ya Exim inalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa Exim Lipa ChapChap, kuwafikia wateja wapya wa Tumaini Health Insurance na Motor Insurance, pamoja na kuongeza idadi ya akaunti za Exim Quick Account zinazofunguliwa. Benki pia inalenga kujenga mahusiano ya muda mrefu na madereva, vikundi vyao na wadau wengine wa sekta ya usafiri kwa ajili ya kuibua fursa za ushirikiano wa baadaye.

Benki ya Exim inawaalika madereva, abiria na wadau wengine wa sekta ya usafiri kutembelea matawi yake nchini kote ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma hizo, kujisajili na kufungua akaunti. Kupitia huduma hizo, benki inalenga kuwasaidia wateja kurahisisha miamala yao, kupata ulinzi wa bima ya afya na vyombo vya usafiri, pamoja na kusimamia fedha zao kwa urahisi.



Kuhusu Benki ya Exim Tanzania

Benki ya Exim Tanzania ilianzishwa nchini mwaka 1997 na hutoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi kupitia mtandao wake wa matawi na huduma za kibenki za kidijitali. Benki hii pia inafanya shughuli zake nchini Comoro, Djibouti na Uganda, pamoja na kuwa na ofisi ya uwakilishi nchini Ethiopia.

No comments:

Post a Comment