Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Thursday, 6 August 2026

BENKI YA NMB YAGEUZA NANENANE KUWA DARASA LA FURSA, MAARIFA NA UWEZESHAJI

DODOMA - Agosti 6, 2026: Benki ya NMB imeendelea kuifanya Nanenane 2026 kuwa zaidi ya maonesho ya kilimo kwa kuendesha kampeni ya utoaji wa elimu ya kifedha, ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa wananchi waliotembelea mabanda yake katika kanda mbalimbali nchini.

Katika Banda la Vijana lililopo Viwanja vya DK John Mwakangale jijini Dodoma, vijana wanaoshiriki mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) walipata mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kubadili mawazo yao kuwa biashara endelevu, kusimamia fedha kwa ufanisi na kutumia huduma za kifedha kukuza shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalungenge, aliwahimiza vijana kulitazama kilimo kama biashara yenye fursa kubwa za kujenga kipato, kuzalisha ajira na kuleta ustawi wa muda mrefu.

Mbali na vijana, maafisa wa NMB waliendelea kutoa elimu kwa vikundi vya wakulima, wafugaji na wajasiriamali waliotembelea mabanda ya benki hiyo. Washiriki walipata uelewa kuhusu huduma mbalimbali za kifedha, mikopo ya sekta ya kilimo, bima pamoja na suluhisho za kifedha zinazowawezesha kuongeza tija, kuimarisha uzalishaji na kupanua biashara zao.

Ushiriki wa NMB katika maonesho ya Nanenane unaakisi dhamira ya benki hiyo ya kuunganisha huduma za kifedha na elimu ya biashara ili kuwawezesha Watanzania kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kupitia elimu, ushauri na huduma za kifedha zinazotolewa katika mabanda yake, NMB imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika wa maendeleo ya wakulima, wafugaji, wavuvi na vijana, huku ikichochea uchumi jumuishi unaojengwa kupitia maarifa, ubunifu na uwekezaji wenye tija.


Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za uhakika kuhusu sekta ya benki, fedha, biashara na maendeleo ya uchumi nchini Tanzania na Afrika.






No comments:

Post a Comment