Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Tuesday, 5 May 2026

BLUE TICKS, RED FLAGS & A COLD GIN: SOMO KUTOKA GORDON’S & TONIC

Dating siku hizi si mchezo—ni kama kazi ya muda wote isiyo na mkataba, likizo wala overtime pay. Mchana unapambana na kazi, usiku unapambana na hisia. Na katikati ya yote hayo, kuna mchezo wa kusoma ishara ambazo mara nyingi hazieleweki.

Leo unaitwa “good morning babe,” kesho uko kwenye blue ticks kama umetuma CV bila referee. Hakuna majibu. Hakuna update. Hata ile “seen with respect” haipo. Unabaki na maswali mengi kuliko majibu, na kadri unavyofikiria, ndivyo unavyochoka zaidi.

Ukweli ni huu—mahusiano mazuri yanahitaji kazi. Na consistency? Hiyo siku hizi imekuwa kama bidhaa ya premium. Si kila mtu anayo.

Watu wanabadilika. Moods zinabadilika. Vipaumbele vinabadilika. Na wakati mwingine, kitu pekee kinachobaki constant ni confusion… ikifuatiwa na maumivu madogo ya moyo ambayo huja bila notice.

Lakini katikati ya kelele zote, kuna vitu vidogo vinavyokupa utulivu. Kama ile baridi ya jioni baada ya siku ndefu. Au funda la kwanza la kinywaji kilichotengenezwa vizuri—kile ambacho hakikupi nafasi ya kukisia.

Hapo ndipo Gordon’s Premix inaingia kimya kimya.

Kuna ile hali ya kufungua chupa na tayari unajua—this is going to be good. Hakuna kubahatisha. Hakuna “leo itakuwaje?” Ni ladha ile ile, ubora ule ule, kila wakati. Tamu. Balanced. Consistent.

Tofauti na baadhi ya connections za siku hizi—hii haina mixed signals.

Baada ya siku ya emails zisizoisha na chats zisizojibiwa, akili inachoka. Unahitaji kitu ambacho hakihitaji effort ya ziada. Hakuna drama. Hakuna kusubiri. Hakuna surprises zisizo za lazima.

Unachofungua, ndicho unachokipata.

Na labda hapo ndipo somo lilipo—hasa kwenye hizi siku za baridi na mvua zinazoendelea.

Consistency si kelele. Si maneno matamu. Si promises nyingi zisizo na delivery.

Ni ile hali ya utulivu—kujua bila kuuliza kwamba kila kitu kiko sawa.

Watu watafanya mambo yaonekane magumu kuliko yanavyopaswa kuwa. Lakini ukweli ni kwamba, si kila kitu maishani kinahitaji kupigania kiasi hicho.

Vingine… vinafanya kazi tu.

Kimya kimya. Bila drama.

Kama ile cocktail yako ya jioni—iliyokwisha pangiliwa vizuri, tayari kwa kufungua na kufurahia.

No comments:

Post a Comment