Foreign Exchange Rates

Equity Bank Advert_12 February 2026

CRDB Bank Advert_070325

Global Sanctions Compliance Masterclass

Saturday, 21 February 2026

BOLT YATOA UFAFANUZI KUHUSU MFUMO WA KAMISHENI NA PUNGUZO KWA MADEREVA TANZANIA

Meneja Mkuu wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole.

Dar es Salaam, Tanzania – Februari 16, 2026 – Kampuni inayoongoza kwa huduma za usafiri mtandao nchini, Bolt, imekutana na waandishi wa habari katika mkutano maalum na wa kina ili kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wake wa kamisheni na punguzo la nauli kwenye app, kufuatia maandamano ya hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya madereva.

Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja Mkuu wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, alieleza kuwa madereva hawabebi gharama za punguzo wanazopewa abiria kupitia ofa za matangazo.

Alifafanua kuwa pale abiria anapopata punguzo — kwa mfano asilimia 40 — abiria hulipa kiasi kilichooneshwa kwenye programu, huku Bolt ikimrejeshea dereva sehemu ya fedha iliyopunguzwa mara baada ya safari kukamilika. Kwa utaratibu huo, dereva hupokea mapato yake kamili ya safari husika bila kuathiriwa na ofa yoyote inayoendelea.

Madereva ni mhimili wa jukwaa letu. Uwezo wao wa kupata kipato cha uhakika na endelevu ni msingi wa mafanikio yetu ya muda mrefu. Tumejizatiti kuendesha mfumo wenye haki na uwazi, unaolinda mapato ya madereva huku ukihakikisha huduma inabaki nafuu kwa abiria,” alisema Kanyankole, akisisitiza kuwa uwazi ni nguzo kuu ya uendeshaji wa kampuni hiyo.

Muundo wa Kamisheni na Ulinganifu wa Kikanuni

Kuhusu muundo wa kamisheni, kampuni ilieleza kuwa inatoza kamisheni ya asilimia 20 — kiwango kilicho ndani ya wigo wa asilimia 15 hadi 25 unaoruhusiwa na Land Transport Regulatory Authority (LATRA).

Aidha, Bolt hutoza ada ya kuhifadhi safari (booking fee) ya asilimia 2 pekee, ambayo huoneshwa wazi kwenye risiti ya kila safari inayokamilika. Licha ya madai ya baadhi ya waandamanaji kuwa kamisheni imeongezwa, kampuni imethibitisha kuwa kiwango cha asilimia 20 kimekuwa kikitumika kwa miaka kadhaa sasa.

Kuimarisha Mawasiliano na Imani ya Wadau

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kampuni kuimarisha mawasiliano ya wazi na vyombo vya habari, madereva na wadau wengine wa sekta, kadri tasnia ya usafiri mtandao nchini inavyoendelea kukua.

Bolt imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwa mshirika wa muda mrefu katika sekta ya usafiri nchini kwa kuzingatia ukuaji wenye uwajibikaji, ulinganifu wa kikanuni na kuimarisha imani ya madereva kupitia uwazi na mawasiliano endelevu.

No comments:

Post a Comment