Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 22 September 2025

NMB YAPOKEA TUZO YA UWAJIBIKAJI WA KIJAMII KATIKA ELIMU KWENYE TUZO ZA MUFTI 2025

Dar es Salaam, Septemba 20, 2025 – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini ikiwemo BAKWATA pamoja na wadau wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia elimu.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mufti za Elimu 2025 zilizofanyika katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuhakikisha elimu si tu inakuza maarifa na ujuzi, bali pia inajikita kwenye malezi yanayojenga tabia njema na uzalendo kwa vijana wa Kitanzania.

Katika hafla hiyo, Benki ya NMB ilitunukiwa Tuzo ya Matokeo Chanya na Uwajibikaji wa Kijamii katika Elimu (Social Impact & Corporate Social Responsibility in Education Award), ikiwa ni heshima kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia na kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu Majaliwa na kupokelewa kwa niaba ya benki na Mkuu wa Idara ya Masoko, Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Rahma Mwapachu.

Kupokea tuzo hii kumeongeza ari ya NMB kuendelea kushirikiana na Serikali, taasisi za dini na wadau mbalimbali ili kuhakikisha elimu inabaki kuwa jumuishi, bora na endelevu—huku ikichangia malezi ya kizazi chenye maarifa na maadili kwa mustakabali wa taifa.



No comments:

Post a Comment