Dar es Salaam, Tanzania – Ijumaa, 19 Septemba 2025: Benki ya Stanbic Tanzania imeandaa hafla maalumu ya HR Summit Dinner katika Hoteli ya Serena, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya benki hiyo. Hafla hiyo iliunganisha viongozi wakuu wa rasilimali watu kutoka sekta mbalimbali kujadili namna ustawi wa kifedha unavyoweza kuleta tija, uaminifu na ukuaji wa taasisi.
Kauli mbiu ya hafla hiyo ilikuwa: “Kuwawezesha Wanaowawezesha Wafanyakazi.” Hafla hiyo iliandaliwa kama jukwaa la kushirikiana na pia kuonyesha jinsi waajiri na benki wanavyoweza kushirikiana kushughulikia changamoto za kifedha zinazowakabili wafanyakazi wengi.
Kauli za viongozi
Mkuu wa Huduma za Wateja Binafsi Stanbic, Bw. Omari Mtiga, alifungua mkutano huo na kusisitiza uhusiano kati ya usalama wa kifedha na kuleta tija kazini:
"Wafanyakazi wanapokuwa salama kifedha, hufanya kazi kwa bidii, huonyesha uaminifu na ubunifu zaidi. Kwa Stanbic, tunaona viongozi wa HR kama washirika muhimu katika kujenga taasisi zenye wafanyakazi wanaostawi."
Kilele cha usiku huo kilikuwa uwasilishaji wa programu ya Employee Value Banking (EVB) uliofanywa na Bw. Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Huduma za Benki Watu Binafsi, na Bw. Priscus Kavishe, Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Uajiri. Programu hii inatoa huduma za kifedha zilizobuniwa kusaidia wafanyakazi kulipa madeni, kupanga maisha ya uzeeni na kukuza akiba. Kwa mujibu wa Stanbic, huduma hizi husaidia kupunguza msongo wa kifedha na kuongeza utulivu pamoja na tija kazini.
Mjadala wa “Financial Fitness at Work”
Kipindi cha mijadala kilichoitwa “Financial Fitness at Work”, kilichoendeshwa na Bw. Elibariki Ndossi, Mkuu wa Uwekezaji, pamoja na Bi. Janeth Mosha, Afisa Uwekezaji, kilijumuisha mjadala mpana kuhusu namna idara za HR zinavyoweza kuingiza ustawi wa kifedha kwenye mipango ya wafanyakazi. Masuala kama vile msongo wa madeni, mipango ya uzeeni, na mapengo ya akiba yalijadiliwa, sambamba na nyenzo za vitendo zinazoweza kutolewa na Stanbic moja kwa moja kwa wafanyakazi.
Usiku huo pia ulipambwa na mawaidha kutoka kwa Bw. Charles Nduku, pamoja na ushuhuda wa wateja waliothibitisha jinsi huduma za kifedha za Stanbic zilivyowasaidia kuboresha taasisi zao.
Hafla ilihitimishwa kwa wito wa Bw. Mahodanga, akiwakaribisha viongozi wa HR kupanga vipindi maalum vya Financial Fitness kwa wafanyakazi wao. Chakula cha jioni na mazungumzo ya kujenga mahusiano yalifuata, yakitoa nafasi kwa wataalamu wa HR na wawakilishi wa Stanbic kuimarisha ushirikiano wao.
Kwa Stanbic, HR Summit Dinner haikuwa tu sehemu ya sherehe za miaka 30, bali pia ni ujumbe dhahiri kwamba benki inajikita katika kusaidia taasisi kuunda nguvu kazi yenye afya, thabiti na imara kifedha.
Mawasiliano
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Jina: Dickson Senzi
Cheo: Meneja Mwandamizi – Mahusiano na Mawasiliano
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Kuhusu Stanbic Bank Tanzania
Stanbic Bank Tanzania ni taasisi inayoongoza katika kutoa huduma za kifedha, ikiwapa wateja binafsi, biashara na taasisi mbalimbali huduma bunifu za kibenki. Kwa kuzingatia uwekezaji endelevu na ushirikiano wa kimkakati, benki inachangia pakubwa kukuza uchumi wa Tanzania na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Stanbic ni sehemu ya Standard Bank Group, benki kubwa zaidi Afrika kwa mtaji, yenye uwepo katika zaidi ya nchi 20. Kupitia mtandao huu, Stanbic inaunganisha Tanzania na fursa za ukuaji Afrika na masoko ya kifedha duniani.
Tovuti: www.stanbicbank.co.tz



No comments:
Post a Comment