Maandalizi ya safari ya mjini yalihusisha kuvaa nguo za “jumapili”, kusafisha viatu, kuamka asubuhi na mapema, kuoga na kujipaka mafuta ya kunukia wewe mwenyewe bila kushurutishwa kwasababu hakukuwa na mtu anataka kwenda mjini mchafu.

Kwa miaka miwili iliyopita tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye Kombe la Shirikisho la TFF ambalo lilipewa jina la CRDB Bank Federation Cup mara baada ya benki ya CRDB kuingia udhamini na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa miaka mitatu na nusu wenye thamani ya TZS 3,255,000,000.
Kwa mara ya kwanza tulishuhudia fainali ya aina yake Juni mwaka jana pale visiwani Zanzibar ambapo Yanga waliweza kutwaa ubingwa kwa kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penati 5-3.

Kombe na kitita
Kivutio kikubwa msimu uliopita kilikuwa ni kombe jipya ambalo lilizinduliwa na benki ya CRDB ambalo lilileta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Kombe hilo lenye pembe za ndovu, mfano wa Mlima Kilimanjaro kwenye kitako chake na rangi ya dhahabu, limewakilisha maliasili za Tanzania kwa marefu na mapana yake.
Mbali na kombe hilo, udhamini huu ulishuhudia wachezaji bora wa mechi wakiondoka na kitita cha Tsh 500,000 kila mmoja kuanzia hatua ya 16 bora huku mchezaji bora wa mechi wa mchezo wa fainali – Ibrahim Bacca akiondoka na kitita cha Tsh 1,000,000.

Mambo mapya!
Msimu mpya wa Ligi umeshuhudia benki ya CRDB ambao ni wadhamini wakuu wakinogesha mashindano haya na kuyaongezea thamani hali ambayo imeleta mvuto kwa mashabiki wa soka nchini.

Mashabiki kukwea pipa
Benki ya CRDB msimu huu imetoa fursa kwa mashabiki watatu kushinda safari iliyolipiwa kila kitu kuongozana na timu bingwa (Yanga SC) kwenye mechi yao ya kwanza ya ugenini ya Klabu Bingwa Afrika. Wadhamini wengi hujikita kwenye timu na wachezaji lakini wanawasahau mashabiki ambao ni sehemu kubwa ya mpira wa miguu. Hivyo kitendo cha kuona benki ya CRDB ikiwakumbuka mashabiki ni cha kupongezwa.

Dau limepanda
Clement Mzize amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mechi ya fainali kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Black Stars. Mzize ameondoka na kitita cha Tsh 2,000,000 ikiwa ni ongezeko la Tsh 1,000,000 kutoka msimu uliopita. Sio yeye tu, lakini wachezaji bora wa mechi za nusu fainali waliondoka na kitita cha Tsh 1,000,000 kila mmoja. Ongezeko la zawadi kwa wachezaji linaongeza sana motisha kwa wachezaji wetu kuendelea kujituma na hatimaye kuwa na mashindano bora.

Sharehe za ufunguzi
Kila aliyefanikiwa kutazama fainali ya mwaka huu kati ya Yanga na Singida Black Stars aidha kwa kuwepo uwanjani au kupitia Azam TV atakuwa shahidi jinsi ambavyo sharehe ya ufunguzi ilinogesha fainali hiyo.

Vijana zaidi ya 100 walioshika bendera kubwa zenye jumbe mbalimbali za fainali hiyo walinogesha sherehe hiyo iliyoshuhudia taa za uwanja zikiwaka na kuzima kwa mpangilio wa sauti ya mziki huku balozi wa benki hivyo kubwa nchini, mwanamuziki Rayvanny akijitokeza kwenye umati wa mashabiki na kutoa burudani ya aina yake. Ama hakika Zanzibar ilifana!

Imebaki misimu miwili ya benki ya CRDB kudhamini mashindano haya ya kombe la Shirikisho la TFF. Tunatamani kujua msimu ujao watakuja na mambo gani mapya kwani wameshatuzoesha kuona vitu vipya kila msimu.
Ubora wa mashindano yetu ya ndani ndio chachu ya maendeleo ya mpira wetu na tuipongeze benki ya CRDB kwa kuongeza thamani ya mashindano haya ambayo yana sifa kubwa ya kuibua vipaji kutoka ngazi za chini kabisa na kuvileta “mjini”
Tukutane msimu ujao wa Kuboli Kiushindani.
Tukutane msimu ujao wa Kuboli Kiushindani.
No comments:
Post a Comment