Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 26 May 2025

BENKI YA UCHUMI YAKABIDHI MKOPO WA MILIONI 326.5 KWA WILAYA YA SIHA KWA AJILI YA VIKUNDI MAALUM

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Uchumi, CPA(T) Samwel Wado, akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Wilaya ya Siha kuhusu utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kutoka mapato ya ndani kupitia Benki ya Uchumi, kwa ajili ya vikundi vya wanawake, vijana na makundi maalum ndani ya Wilaya ya Siha.
Mkuu wa Wilaya ya Siha, Mhe. Dkt. Christopher Timbuka, akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, serikali na wawakilishi wa vikundi, ameitaka Benki ya Uchumi kuendeleza ushirikiano wa karibu na serikali ili kuwawezesha wananchi kupitia vikundi vyao.

Aidha, amewahimiza wananchi kutumia fedha hizo kwa ajili ya uwekezaji endelevu, huku akisisitiza umuhimu wa kuzirejesha kwa wakati. Amesisitiza kuwa ni lazima kufanya kazi kwa bidii na kutumia vyema mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia wananchi mmoja mmoja na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Siha, Mei 23, 2025: Benki ya Uchumi imekabidhi rasmi mkopo wa shilingi milioni 326.5 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwa ajili ya kuwawezesha vikundi vya wanawake, vijana na makundi maalum kiuchumi. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Wilaya ya Siha, ikihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Dkt. Christopher Timbuka.


Mkopo huo usio na riba umetolewa kupitia mpango wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri, kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhakikisha kuwa makundi maalum yanashirikishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Lengo kuu ni kuchochea maendeleo ya vikundi vya kijamii na kuinua hali ya maisha ya wananchi kwa ujumla.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Timbuka aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na fursa hiyo adhimu. "Fursa hii haijaletwa kwa bahati mbaya. Ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau kama Benki ya Uchumi kuhakikisha wananchi wetu wanapata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya kuendeleza miradi yao ya kiuchumi," alisema Dkt. Timbuka.


Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Uchumi, CPA(T) Samwel Wado, akizungumza mbele ya Mgeni Rasmi katika mkutano huo, alieleza jinsi benki hiyo inavyoshirikiana kwa karibu na Serikali katika kuwawezesha wananchi kufikia maendeleo endelevu. Alifafanua kuwa Benki ya Uchumi imeweka njia salama na rahisi za upatikanaji wa mikopo kwa vikundi mbalimbali, na itaendelea kutoa mikopo hiyo kwa vikundi vilivyobaki ndani ya Wilaya ya Siha.

Benki ya Uchumi itaendelea kuwa mshirika wa kweli wa Serikali katika jitihada za kuinua uchumi wa wananchi. Tunahakikisha kuwa kila kundi linalengwa linapata mkopo kwa wakati na kwa masharti rafiki,” alisema CPA Wado.

Mpango huu ni hatua muhimu kuelekea kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuondoa vikwazo vya kifedha vinavyowakabili vijana, wanawake na makundi maalum.

No comments:

Post a Comment