Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Wednesday, 5 March 2025

VODACOM YAZINDUA DUKA LA HUDUMA KWA WATEJA NUNGWI, ZANZIBAR


Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Vodacom imezindua duka jipya la huduma kwa wateja kata ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini A, ikiwa ni hatua muhimu ya kutoa huduma bora za mawasiliano na bidhaa za kisasa kwa wakazi wa eneo hilo. 


Duka hilo lilizinduliwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini A, Mariam Khamis, akishuhudiwa na mdau wa Vodacom, Saleh Judas na Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo, Brigita Shirima. 


Uzinduzi huu ni hatua mojawapo ya Vodacom kupanua huduma zake visiwani humo ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi.


No comments:

Post a Comment