Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Tuesday, 4 March 2025

STANBIC YADHAMINI KONGAMANO LA MAENDELEO YA WANAWAKE, USHIROMBO MKOANI GEITA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Dk. Doroth Gwajima (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Stanbic Tanzania, Peter Bitesigilwe, wakati akiwasili katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ushirombo, katika Kongamano, kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita. Benki ya Stanbic ilikuwa mdhamini mkuu wa kongamano hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela.

Ushirombo - Geita, 2 Machi 2025: Benki ya Stanbic Tanzania imedhamini Kongamano la Maendeleo ya Wanawake katika Halmashauri ya Ushirombo mkoani Geita ikiwa sehemu ya kuelekea kilele cha wiki ya wanawake.

Akizumgumza kwenye kongamano hilo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt Dorothy Gwajima alisema kutukutanisha katika kongamano hili maalum la kutambua mchango wa wanawake wa mkoa wa Geita na Tanzania nzima kwa ujumla katika maendeleo ya Taifa letu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Dk. Doroth Gwajima (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Stanbic Tanzania, Fredrick Max, wakipiga picha ya kumbukumbu katika Kongamano kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, lililofanyika Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita. 
 
Natambua kuwa kongamano hili ni sehemu ya matukio kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kitaifa yatafanyika jijini Arusha na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan.

Tunakutana leo kwa dhamira moja kuu – kuhakikisha kuwa maendeleo ya wanawake yanapewa msukumo unaostahili katika taifa letu. Katika muktadha huu, tunatazama nyuma kuona tulipotoka, lakini muhimu zaidi, tunajikita kwenye mwelekeo wa mbele kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa fursa zote za kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu. Pia Niwashukuru Benki ya Stanbic kwa kutuwezesha kufanikisha kongamano hili na kuweza kuleta fursa kwa wananchi wa Geita na niwaombe mabenki mengine waige kutoka benki hii.


Afisa Mkuu wa Idara ya Biashara wa Stanbic Tanzania -Fredrick Max, alisema, Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitilia mkazo kuwa jukumu la kuwainua wanawake ni jukumu letu sote, serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.

Sisi Benki ya Stanbic tunatekeleza azma hii kwa vitendo kwa kutoa mikopo nafuu tukijikita kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.

Katika Stanbic kupitia kauli mbiu ya mwaka huu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” Safari ya Maendeleo ya Wanawake tunaizingatia zaidi ndio maana tumeweza kuwa progamu maalum, Kama programu ya Ignite women au “kuwasha wanawake” ambao umelenga kuwawezesha wanawake kuwa na uwezo wa kuongoza na kujiamini, hivyo basi Benki ya Stanbic inajivunia kuwa sehemu ya safari hii na tunaamini tukiwainua wanawake tunaliwezesha Taifa letu.

Katika kipindi hiki, tumeendelea kukua kwa kasi na sasa ni benki namba tatu nchini kutokana na ripoti ya hesabu za mwaka 2024. Katika kipindi hiki chote tumekua mshirika wa kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wateja na jamii zinazotuzunguka, na kubwa zaidi tunajivunia ushiriki wetu katika kuchangia ufanikishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya Taifa letu katika sekta mbalimbali za Uchumi.

Benki yetu imeendelea kukua kwa kasi tukihudumia Watanzania kupitia matawi yetu 11, na mengine sita yakiwa mbioni kufunguliwa mwaka huu moja kati ya hayo likiwa mkoani Geita.

Lakini pia tuna mawakala zaidi ya 1,500 waliotapakaa nchi nzima, na tunatoa huduma bora za benki kidijitali. Ukuaji huu unaendana na ukuaji wa idadi ya wafanyakazi wetu ambao sasa kwa ujumla wetu tupo zaidi ya 600 nchi nzima.

Na mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela alihitimisha kusema, Taasisi ya fedha ya Stanbic inajishughulisha kwa kiwango kikubwa sana na shughuli za wanawake. Tunaishukuru sana Benki ya Stanbic kwa ushirikiano wenu na namna ambavyo mmewezesha jambo hili.

No comments:

Post a Comment