Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. |
Dar es Salaam, Machi 20, 2025: Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari jana aliongoza mamia ya Waislamu ambao ni wateja wa benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo huku akisisitiza umuhimu wa taasisi za fedha nchini kuzingatia mahusiano na huduma zinazo heshimu sheria, imani na misingi ya dini za wateja.
Kwa upande wake Bw Sabi alisema benki hiyo imekuwa ikiutambua mwezi wa Ramadhani kuwa ni nguzo muhimu ya imani ya Kiislamu, wakati wa ibada, upendo, na sadaka hivyo imekuwa ikiutumia kama ishara yake ya msingi katika kuthibitisha mahusiano yake na wateja pamoja na wadau wote wa benki hiyo ikiwemo serikali lengo likiwa ni kushirikiana pamoja baraka za mwezi huo.
“Hivyo kipekee kabisa niwashukuru nyote kwa kuendelea kuiamini Benki ya NBC kama mshirika wenu wa kifedha. Tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu, ikiwemo akaunti za La Riba zinazofuata taratibu za ‘Sharia’ ili kufikia mahitaji yenu ya kibenki. Nichukue pia fursa hii kuwakaribisha kutumia huduma yetu iliyoboreshwa ya ‘NBC Kiganjani’ ambayo ni huduma ya kibenki kwa simu za mkononi.’’ Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu NBC Kiganjani iliyoboreshwa Sabi alisema: “Kupitia NBC Kiganjani sasa mteja anaweza kufungua akaunti yeye mwenyewe, kufanya malipo ya serikali (GEPG), kununua LUKU, na kufanya malipo kupitia NBC Lipa Namba na huduma mpya ya Edu-Connect kwa ajili ya malipo ya ada za shule’’
Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa. Kwa wateja wa Kiislamu wa benki ya NBC jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilikuwa fursa nzuri ya kufurahi pamoja na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment