![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzo2C2gHQ68iKp5R6mZqYBI2Y8jQfflzes2k3WQ4Vzdpu0UNeYhbIBH-si0So0j_lgSYxTYi2TUGnHoQVkypd-s_afIYjrcvERsVg0KlDByBBO7pSczxavfWOl4a4TF8hRiN_xKevsCxYGXP4UIPkCje3Te-5bjE3Vv0cW1uFxwSqmcDaGmR01USiQfEKr/w640-h426/WhatsApp%20Image%202025-02-14%20at%2016.05.23.jpeg)
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa kuahidi kuendelea kuwekeza katika uvumbuzi wa kidijitali na kuongeza ubora wa huduma kwa wateja wake na kuwa wanayo dhamira ya kuimarisha nafasi ya TCB katika sekta ya kibenki nchini.
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ilianzishwa mwaka 1925 wakati wa utawala wa kikoloni kwa jina la Tanganyika Post Office Savings Bank. Baada ya uhuru, benki hiyo ilibadilishwa kuwa Tanzania Postal Bank mwaka 1992, kabla ya kubadilishwa kuwa Tanzania Commercial Bank (TCB) mnamo mwaka 2021. Kupitia mageuzi hayo, benki imeendelea kukua na kuwa moja ya taasisi muhimu katika sekta ya fedha nchini Tanzania.
Katika kuadhimisha miaka 100, TCB ilizindua kampeni ya Mahaba Kisiwani kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki za kidijitali. Kupitia kampeni hiyo, wateja waliotumia njia za kidijitali kufanya miamala walijishindia safari ya kupumzika Zanzibar.
Mmoja wa washindi wa kampeni hiyo, mfanyabiashara Maygrace Nyambuka, aliipongeza TCB kwa huduma zake bora, akieleza kuwa miamala ya kidijitali imerahisisha biashara yake na kumpunguzia gharama za kutuma na kupokea fedha.
Mustakabali wa TCB
Katika hatua inayofuata, TCB inatarajia kuendelea kuwekeza katika mifumo ya teknolojia ya kifedha, kuongeza mtandao wa matawi na wakala wa benki, na kuimarisha huduma za mikopo kwa wateja wa sekta mbalimbali.
Kwa miaka 100 ijayo, TCB inalenga kuwa benki ya kidijitali inayoongoza nchini Tanzania, ikiwa na dhamira ya kutoa huduma za kifedha zinazofikia kila Mtanzania kwa gharama nafuu na kwa ufanisi wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment