Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Tuesday, 11 February 2025

STANBIC YATOA ELIMU YA UJUZI WA FEDHA KWA WATOTO WA WATEJA WAO MWANZA

Meneja wa Huduma Binafsi, Biashara na Masoko wa Benki ya Stanbic, Victoria Kimaro akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya ujuzi wa kifedha ya Benki ya Stanbic. Benki ya Stanbic ilitoa elimu kwa zaidi ya watoto 15 wa wateja wake kuhusu ujuzi wa kifedha. Tukio hili lilifanyika jijini Mwanza.
Mshauri wa Uwekezaji kutoka Benki ya Stanbic, Richard Ndisi akitoa elimu kwa watoto wa wateja wa benki hiyo kuhusu ujuzi wa kifedha. Tukio hilo lilifanyika kwa lengo la kudumisha utamaduni wa Benki ya Stanbic wa kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa watoto wa wateja wao, ili kuwawezesha kupata maarifa na ujuzi huo.

Elimu ya Ujuzi wa Fedha ya Benki ya Stanbic Tanzania inaendelea kuhimiza utoaji wa elimu ya fedha kupitia mpango wake wa kipekee unaolenga kuwapa familia stadi muhimu za usimamizi wa fedha. Mpango huu unawalenga watoto kwa kuwaelimisha kuhusu jinsi ya kupata, kutumia, kuweka akiba, na kutoa pesa kwa uwajibikaji, huku ukiwaimarisha katika nidhamu ya kifedha tangu utotoni. Kwa kushirikisha familia katika mbinu shirikishi na za kufurahisha za kujifunza, Benki ya Stanbic inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kujenga kizazi chenye uelewa mzuri wa masuala ya fedha na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yao ya baadaye.


Safari hii, utoaji wa elimu ya Ujuzi wa Fedha umefanyika katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza, ikiwa ni maalum kwa wateja wa huduma za Benki binafsi pamoja na familia zao. Tukio hili liliwapa watoto wa wateja fursa ya kushiriki katika shughuli za kuvutia kama vile michezo ya bajeti, mazoezi ya uigizaji wa majukumu, na majadiliano ya kina kuhusu misingi ya fedha. Kwa kuleta mpango huu jijini Mwanza, Benki ya Stanbic imethibitisha tena kujitolea kwake kupanua elimu ya fedha, kuhakikisha kuwa familia nyingi zaidi kote Tanzania zinapata ujuzi muhimu wa usimamizi wa fedha.

No comments:

Post a Comment