“Wakati tukiwahakikishia wateja wa NMB muendelezo bora wa huduma bora na rafiki kwao, sisi tunaamini kwamba kila Mtanzania anapaswa kuwa na akaunti NMB, Benki Bora kwa miaka 11 mfululizo katika miaka 12 iliyopita,” alisema Mponzi huku akiinadi Akaunti ya Wekeza yenye riba hadi asilimia 12 kwa mwaka.
Ukiondoa Shilingi Milioni 100, katika fainali hiyo walitafutwa washindi saba wa pikipiki ya mizigo ya matairi matatu (moja kwa kila mmoja), mshindi mmoja wa trekta ya kilimo ‘power tiller,’ huku washindi wengine wanne kila mmoja akijinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 5.
Kupitia kampeni hiyo, washindi 10 wa kila wiki walijishindia fedha taslimu Sh. 100,000 kila mmoja, huku washindi wengine tisa wakijinyakulia kimoja kati ya Friji, Televisheni ya kisasa, mashine ya kufulia na jiko la gesi, kulingana na matakwa ya mteja.
Katika zawadi za droo za kila mwezi, benki hiyo ilikuwa ikiwazawadia washindi wanne wa kila mwisho wa mwezi Sh. Mil. 5 kila mmoja, ikiwa na maana wateja wanane katika miezi miwili ya ya NMB Bonge la Mpango, waliojizolea Sh. Mil. 40 kwa wote (wakiwemo wanne waliopatikana kwenye fainali).
NMB Bonge la Mpango ilianza mwaka 2021, kabla ya mwaka uliofuata (2022) kurejea tena kwa kampeni hiyo ikitumia kaulimbiu ya ‘2merudi Tena,’ kisha mwaka jana 2023 kuitwa NMB Bonge la Mpango ‘Moto Ule Ule’ na mwaka huu kuwa NMB Bonge la Mpango ‘Mchongo Nd’o Huu.’
No comments:
Post a Comment