Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 15 November 2024

BENKI YA TCB YAZINDUA LIPA POPOTE KURAHISISHA MALIPO KWA WAFANYABIASHARA


Dar es Salaam, Tanzania – 13/11/2024 – Benki ya Biashara Tanzania (TCB) inajivunia kutangaza uzinduzi wa bidhaa ya LIPA POPOTE, suluhisho la malipo lililobuniwa ili kurahisisha miamala kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) na wamiliki wa biashara. Bidhaa hii mpya inawawezesha wateja wa Benki ya TCB kupokea malipo moja kwa moja kwenye akaunti zao za benki kupitia namba moja ya mfanyabiashara iitwayo LIPA POPOTE. Zaidi ya hayo, wenye akaunti katika Benki ya TCB wataweza kulipia bidhaa na huduma kwa urahisi wakitumia namba maalum ya muuzaji (Till Number), hivyo kufanya miamala iwe rahisi zaidi kuliko hapo awali. 


LIPA POPOTE imebuniwa kushughulikia hitaji la malipo ya kifedha linaloongezeka kwa kasi nchini miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) ambao ni uti mgongo wa uchumi wa taifa. Suluhisho hili linalenga kurahisisha mchakato ya malipo kwa wamiliki wa biashara, kuwawezesha kupokea malipo papo hapo na kwa usalama. Bila kuhitaji gharama za usajili, huduma hii inapatikana kirahisi, ikiongeza wigo wa ujumuishi wa kifedha kwa kuondoa vizuizi vya miamala ya kidijitali kwa biashara mbalimbali kote nchini. 


TCB tumekusudia kukuza ubunifu unaogusa maisha ya Watanzania. LIPA POPOTE inadhihirisha dhamira yetu ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) kwa kutoa suluhisho bora kwa malipo rahisi na salama,” alisema Bw. Jesse Jackson, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali na Ubunifu wa Benki ya TCB. 


LIPA POPOTE ni zaidi ya njia ya malipo; ni hatua kuelekea uwezeshaji wa kiuchumi kwa wafanyabiashara nchini, kuanzia mijini hadi jamii za vijijini. Lengo letu ni kuzifanya huduma za kifedha ziwe salama, nafuu na zipatikane kwa watu wote,” alisisitiza Bw. Jesse Jackson. 


Kwa kuzindua suluhisho la kidijitali la malipo kama vile LIPA POPOTE, tunaboresha kikamilifu malengo ya Tanzania ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wafanyabiashara, watu binafsi na jamii ambazo hazijafikiwa bado. Njia hii ya malipo inatarajiwa kubadilisha namna biashara ndogo zinavyofanya kazi, na kurahisisha miamala ya kifedha,” alifafanua Bi. Lilian Mtali, Mkurugenzi wa Biashara kwa Wateja Wadogo na wa Kati, TCB. 


"Tunashuhudia mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kuboresha uchumi wetu kila kukicha, TCB inalenga kuwa mstari wa mbele katika kutoa masuluhisho ya kibenki yenye ubunifu na kuchochea ujumuishi wa kifedha kwa wote," aliongeza Adam Mihayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Tanzania. "LIPA POPOTE ni uthibitisho wa dhumuni letu la uwezeshaji uchumi na upatikanaji wa huduma za kifedha, ili kuwanufaisha Watanzania wote na huduma za kisasa za kibenki."





No comments:

Post a Comment