Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiongoza kikao kati yake na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma. |
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akifafanua jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma. |
Na. Benny Mwaipaja, Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma, ambapo walijadili kuhusu mchango wa Sekta ya Benki katika uchumi wa nchi kupitia huduma jumuishi za kifedha.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, wakati ujumbe wa TBA uliongozwa Mwenyekiti wake, Bw. Theobald Sabi.
No comments:
Post a Comment