Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Wednesday, 30 October 2024
Monday, 28 October 2024
NMB KUWEZESHA MAKAMPUNI YA KOREA KUSINI YANAYOTEKELEZA MIRADI NCHINI
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB Linda Teggisa wakati ya semina ya ‘2024 Korea – Tanzania Project Plaza’ iliyofadhiliwa na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam na kukutanisha zaidi ya kampuni 100 jijini Dar es Salaam na mtandaoni.
Teggisa aliongeza, "Tunatarajia kupanua wigo wetu kwa kutoa huduma zingine ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa mitaji, ufadhili wa mali na masuluhisho ya miamala ili kuongeza mnyororo mzima wa thamani wa miradi."
“Mfumo imara kwa kiasi kikubwa umechangia ukuaji wa sekta ya benki na fedha katika miaka ya hivi karibuni. Sekta ya benki imeshuhudia ukuaji mkubwa katika utoaji wa mikopo kutoka shilingi trilioni 34.6 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 46 kwa mujibu wa ripoti,” alisema.
Alibainisha kuwa benki yake itaendelea kuchukua jukumu kuu katika kukuza ushirikishwaji wa kifedha kama sehemu ya juhudi za kuziba pengo kwa wasio na akaunti za benki.
Teggisa wakati wa hafla hiyo alipongeza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Korea Kusini na kuongeza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kukuza maendeleo.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri wakati wa hafla hiyo rai kwa makampuni zaidi ya Korea Kusini kuja kuwekeza hapa nchini.
NMB COMMITTED TO FINANCING S. KOREAN FIRMS EXECUTING PROJECTS IN TANZANIA
The NMB Bank Head Transaction Banking, Linda Teggisa reaffirmed this during an interactive hybrid session sponsored by NMB Bank held in Dar es Salaam dubbed, “2024 Korea – Tanzania Project Plaza’ that brought together over 100 companies in Dar es Salaam and online.
Teggisa added, “We expect to extend other services including capital financing, asset financing and transactional solutions to cover the entire value chain of the projects.”
She noted that NMB Bank will continue to be a strong player in project financing through partnerships with global financial institutions and commended the sixth phase Government for creating a conducive business environment.
She noted that NMB Bank will continue playing a leading role in driving financial inclusion as part of efforts to bridge the no banked gap.
During the event, Teggisa commended the long-term relationship between Tanzania and South Korea adding that the ties between the two countries have continued to foster development.
Earlier, the Tanzania Investment Center (TIC) Executive Director, Gilead Teri during the event lured more South Korean firms to come and invest in Tanzania.
Saturday, 26 October 2024
BANDARI YA MTWARA KUSHUGHULIKIA SHEHENA YOTE YA KOROSHO
Mtwara: Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetangaza kuwa Bandari ya Mtwara ipo tayari kushughulikia shehena yote ya korosho kwa ajili ya mauzo ya nje katika msimu wa sasa wa uuzaji.
Hii ni kufuatia agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba bandari hiyo itumike kama njia kuu ya kusafirisha korosho ghafi kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania kwenda katika masoko ya kimataifa.
Akizungumza alipokuwa katika ziara yake mkoani Mtwara mnamo Septemba mwaka jana, Rais Samia alisisitiza kuwa usafirishaji wa korosho kupitia bandari nyingine unatakiwa upate kibali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa. Akizingatia agizo hilo, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi, alisema kuwa bandari hiyo sasa imeboreshwa na ipo tayari kushughulikia shehena yote ya korosho msimu huu.
“Msimu uliopita, baada ya agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, tuliweza kusafirisha tani 253,000 za korosho na kushughulikia jumla ya meli 28. Mwaka huu, tumejiandaa zaidi kushughulikia mazao ya korosho. Kwa ufupi, tuko tayari kabisa,” alisema Bw Nyathi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari siku ya Ijumaa.
Maandalizi ya bandari yameimarishwa na upatikanaji wa vifaa vipya, ikiwa ni pamoja na kreni mbili za rununu, mashine ya kushughulikia makasha matupu, “reach stackers”, na Tag Boats za kisasa. Vifaa hivi vimeboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wa kuhudumia makontena katika bandari hiyo.
“Vifaa hivi vipya vimetuwezesha kujiweka katika nafasi bora zaidi ya kusafirisha korosho zote ambazo Tanzania itauza nje msimu huu,” alisema Bw Nyathi kwa furaha.
Kwa kuwa msimu wa mauzo ya korosho tayari umeshaanza, makontena takriban 3,700 yapo tayari katika Bandari ya Mtwara kushughulikia usafirishaji wa korosho. Bw Nyathi aliongeza kuwa, kwa ushirikiano na sekta binafsi ambayo inamiliki Maeneo ya Makontena ya Ndani (ICDs), bandari hiyo ina makontena mengine 800 ambayo yanaweza kutumika. Upakiaji wa korosho kwenye makontena unaendelea.
Maboresho haya katika Bandari ya Mtwara ni habari njema kwa wakulima wa korosho, ambao wameona ongezeko la bei katika minada ya karibuni. Kwa mfano, katika mnada wa kwanza uliofanyika tarehe 11 Oktoba, ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (Tanecu), tani za ujazo 3,857 za korosho ghafi ziliuzwa kwa bei kati ya Sh4,035 na Sh4,120 kwa kilo. Mnada wa pili uliofanyika tarehe 12 Oktoba, ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwamba (LMCU), uliuza tani za ujazo 6,435 kwa bei kati ya TZS 3,400 na Sh3,865 kwa kilo.
Ili kuvutia zaidi wauzaji nje, Bw. Nyathi alitangaza kuwa bandari hiyo imefuta gharama zote za kuhifadhi makasha yenye korosho kwa msimu mzima wa mauzo.
“Hapo awali, kuhifadhi makasha ilikuwa bure kwa kipindi maalum, na baada ya hapo gharama za kuhifadhi zilianza kutozwa. Hata hivyo, kwa msimu huu, kuhifadhi ni bure kabisa kwa msimu mzima wa korosho,” alieleza.
Bw Nyathi alihakikisha pia kwamba usimamizi wa korosho hautaathiri shughuli nyingine za mizigo katika bandari hiyo, ikiwemo bidhaa kama mkaa na saruji. “Tunatarajia meli tatu zaidi kufika bandarini wiki hii, zikiwa na makontena zaidi,” alisema.
Alisisitiza kuwa Bandari ya Mtwara ipo katika eneo muhimu kijiografia kwa wateja wa TPA katika mikoa ya kusini na nchi jirani, akibainisha kuwa maboresho hayo yamewezeshwa na uwekezaji mkubwa wa serikali katika miezi ya karibuni.
Friday, 25 October 2024
MTANZANIA ACHAGULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA
Benki ya Dunia, imemchagua Mtanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita.
Uamuzi wa Dkt. Kibwe kuikwaa nafasi hiyo nyeti katika Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, umetangazwa katika Mkutano wa Mwaka wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Benki ya Dunia, uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia inafanyika.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, Dkt. Kibwe alihudumu katika Ofisi hiyo ya Bodi kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mshauri na Mshauri Mwandamizi kwa zaidi ya miaka saba, tangu mwaka 2017.
Akizungumza Jijini Washington D.C, baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe amesema kuwa ataitumia nafasi hiyo kusimamia uendeshaji wa Benki na Taasisi zake Pamoja na kutetea Maslahi ya nchi katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia pamoja na maslahi ya Kanda ya Afrika anayoisimamia ili kukuza maendeleo na uchumi wa nchi hizo.
NMB, IFC & MASTERCARD PARTNER TO ENHANCE FINANCIAL ACCESS FOR WOMEN IN TANZANIA
NMB Bank Plc has partnered with the International Finance Corporation (IFC) and Mastercard to launch the "Banking on Women Advisory Project." This initiative aims to enhance their existing Jasiri Proposition to better attract, retain, and grow women-led businesses in Tanzania.
NMB Bank Plc believes every woman in Tanzania deserves access to the financial tools necessary for success. Gender equity and economic empowerment are at the forefront of their strategic priorities. This partnership represents a crucial step in their gender inclusion strategy, reinforcing their commitment to addressing the unique financial challenges women face.
NMB, IFC NA MASTERCARD WAINGIA MAKUBALIANO KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WANAWAKE NCHINI
Benki ya NMB imesaini makubaliano na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) na Mastercard kuzindua Mradi wa Ushauri wa “Banking on Women Advisory Project," ambao unalenga kuboresha masuluhisho ya kifedha kwa wanawake nchini Tanzania.
BENKI YA DCB YAJA NA MIKOPO YA PIKIPIKI NA BAJAJI YENYE MASHARTI NAFUU
Benki ya Biashara ya DCB imezindua mikopo ya boda boda na bajaji yenye masharti nafuu, ikiwa na lengo la kuwaondolea adha na usumbufu vijana wanaojishughulisha na biashara ya usafiri wa boda boda wanayoipata kutoka baadhi ya watu wanaotoa mikopo yenye masharti magumu maarufu kama ‘mikopo umiza ama kausha damu’.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbagala, Temeke, jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Bw. Ramadhan Mganga akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wake Bw. Sabasaba Moshingi alisema, mikopo hiyo huwafanya vijana wakiiishi kwa hofu na mashaka na kijikuta muda wote wakiendesha pikipiki bila tahadhari hivyo kuhatarisha usalama wao na abiria zao.
“Mtu anakupa pikipiki anakupa marejesho ya zaidi ya miezi 14, unatoa elfu 12 kwa siku, unajikuta umelipa zaidi ya shs milioni 4.5 kwa pikipiki moja, sasa sisi DCB tukasema haiwezekani vijana hawa wa kitanzania waishi kwa hofu na maumivu.
ADVANCING FINANCIAL SERVICES THROUGH INNOVATIVE LENDING SOLUTIONS
CEO of Tausi Africa Technologies, Derick Kazimoto (left) and CEO of Creditinfo Tanzania, Edwin Urasa during the launch. |