Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Friday, 25 October 2024
BENKI YA DCB YAJA NA MIKOPO YA PIKIPIKI NA BAJAJI YENYE MASHARTI NAFUU
Benki ya Biashara ya DCB imezindua mikopo ya boda boda na bajaji yenye masharti nafuu, ikiwa na lengo la kuwaondolea adha na usumbufu vijana wanaojishughulisha na biashara ya usafiri wa boda boda wanayoipata kutoka baadhi ya watu wanaotoa mikopo yenye masharti magumu maarufu kama ‘mikopo umiza ama kausha damu’.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbagala, Temeke, jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Bw. Ramadhan Mganga akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wake Bw. Sabasaba Moshingi alisema, mikopo hiyo huwafanya vijana wakiiishi kwa hofu na mashaka na kijikuta muda wote wakiendesha pikipiki bila tahadhari hivyo kuhatarisha usalama wao na abiria zao.
“Mtu anakupa pikipiki anakupa marejesho ya zaidi ya miezi 14, unatoa elfu 12 kwa siku, unajikuta umelipa zaidi ya shs milioni 4.5 kwa pikipiki moja, sasa sisi DCB tukasema haiwezekani vijana hawa wa kitanzania waishi kwa hofu na maumivu.
“Lakini pia tunazindua mikopo hii ya pikipiki na bajaji, ili pia kuunga mkono juhudi za serikali yetu inayoongozwa na Rais, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan katika azma yake ya kuendelea kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa vijana. Tutaendelea kusapoti juhudi zote za serikali na tupo tayari wakati wowote kuitikia wito tutakapotakiwa kufanya hivyo”, alisema Bwana Maganga.
Akizungumza zaidi kuhusu mikopo hiyo, Mkurugenzi huyo alisema mikopo ya pikipiki na bajaji imepata uitikio mkubwa kutoka kwa vijana kwani kwa kipindi kifupi zaidi ya shs bilioni 1.5 zimekopeshwa huku wakitarajia kutoa kiasi cha zaidi ya shs bilioni 5 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Bw. Abdallah Mtinika, aliipongeza Benki ya DCB Kwa kuja na huduma hiyo akisema kuwa mikopo hiyo imelenga kundi sahihi lenye uhitaji.
“Benki ya DCB ni Benki yetu, ilianzishwa na halmashauri za Dar es Salaam, wanahisa waanzilishi wakiwa Halmashauri za Temeke Kinondoni na Ilala, nina furaha kubwa kuona benki hii ikisonga mbele.
“Nawaasa vijana wenzangu nendeni mkachape kazi, rudisheni mikopo yenu kwa wakati ili muweze kutunza heshima yangu na naambiwa kuna vijana zaidi ya 300 wameshanufaika na mikopo hii, nitafurahi endapo nitaitwa tena kushuhudia kundi la vijana wengine wakipokea mikopo ya boda boda.
“Kwa namna ya kipekee niwaase pia kama mfahamuvyo hiki ni kipindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, kujiandikisha kwenu ni ishara kuwa mnataka kuweka viongozi wazuri, mjitokeze kushiriki katika harakati zote za uchaguzi ili muweze kutuletea viongozi bora kwa mustakabali mzuri wa Taifa letu”, alisema Meya huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment