Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 19 August 2024

WATEJA WA VODACOM WAENDELEA KUSHINDA, MMOJA APATA SH. MIL. 20

Ni Balaa! Kila Mtu ni Mshindi! Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania Plc, George Venant (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh.20,000,000/- mshindi wa kwanza wa kipengele kikuu wa droo ya kampeni ya ‘Ni Balaa!’, Bankason Yusuph wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali, iliyofanyika tarehe 16 Agosti 2024, jijini Arusha.
Ni Balaa! Meneja Mauzo Mkoa wa Kilimanjaro, Sifa Msuha (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh.500,000/- mshindi wa droo ya pili ya mwezi, Agripina Pius wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali, iliyofanyika tarehe 16 Agosti 2024, jijini Arusha. Kulia ni George Venant, Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania Plc.

Arusha: Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania (PLC) imetoa zawadi kwa washindi wa kampeni mpya ya ni Balaa kila mtu ni mshindi, ikiwemo mshindi mkuu Sh.20,000,000 na Sh.500,000 kwa washindi watano baada ya kushinda kwenye droo ya kampeni hiyo kwa mikoa ya Kaskazini.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom, George Venant, amekabidhi zawadi kwa mshindi mkuu Bankason Yusuph, kiasi cha Sh.20,000,000 Mkoani arusha, akiwa ni mshindi wa zawadi kuu wa kwanza kupatikana kwenye kampeni hiyo mpya ya ni Balaa kila mtu ni Mshindi, wakifuatiwa na shindi wengine ambayo imeanza rasmi Agosti nne mwaka huu.

George amesema kampeni hiyo ina lengo la kunufaisha wateja na jamii kwa ujumla na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushinda zawadi za kila siku, wiki na mwezi, pamoja na washindi watano wa zawadi kuu.

Kwa upande wao washindi wa kampeni hiyo wakaelezea furaha zao, pamoja na jinsi watavyotumia fedha walizokabidhiwa kufikia ndoto zao.

Kampeni hiyo iliyobebwa na kaulimbiu ya “Kila Mtu ni Mshindi”, itaendelea hadi Oktoba, ambapo kwa upande wa Washindi wa kila siku watapata Sh.100,000, washindi wa kila wiki Sh.500,000, washindi wa kila mwezi Sh.1,000,000 na washindi watano wa zawadi kuu kila mmoja atapata Sh.20,000,000.

No comments:

Post a Comment