Balozi wa Kampeni ya Kijiditali ya Tap Tap Utoboe ya Exim Bank Tanzania, Idris Sultan (kati) akitangaza washindi 10 wa droo ya pili ya mwezi yenye lengo la kuwahamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala yao ya malipo kwa kutumia simu za mkononi na mtandao ili kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, pikipiki, bajaji na gari mpya. Kushoto ni Thuweiba Bakary, Afisa wa benki hiyo kutoka Idara ya Huduma Mbadala za kibenki na Kidijitali, na Lucy Katamba, Mkaguzi na Mdhibiti wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania wakiwa katika droo hiyo iliyofanyika tarehe 16 Agosti, 2024 katika Tawi la Exim Bank Masaki jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment