Takwimu hizo zimemfurahisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na akiwa kwenye banda la maonyesho la NMB amesema ‘Kazi Iendelee’ kauli ambayo huitumia anapokubaliana na jambo hasa kwenye miradi ya maendeleo.
“Mheshimiwa Rais tunakupongeza sana katika maoni yako hasa ya kuwainua wakulima na wafugaji nchini, na sisi NMB tunayo mikakati ya kusaidia sekta ya kilimo na mifugo ambako tumeona kuna mapinduzi makubwa,” amesema Zaipuna.
Mtendaji Mkuu ameeleza kuwa kati ya mikopo iliyotolewa, Shilingi bilioni 450 zimetolewa kwenye mpango wa riba nafuu ya asilimia 9 ambako ndiko waliko wakulima na wafugaji.
Zaipuna amesema benki hiyo imeanzisha mkakati maalumu wa kuwafikia wakulima na wananchi kupitia mpango wake wa kufungua akaunti za Shilingi 1,000 ambako mamilioni ya Watanzania wamejiunga huko hivyo kuwawezesha wananchi kupata mikopo kwa urahisi.
“Mheshimiwa Rais akaunti hii imerahisisha wananchi na wakulima kupata mikopo kwa njia ya mtandao (Mkopo fasta) bila kuweka foleni benki na mikopo hiyo inaanzia kiasi cha Shilingi 1,000 hadi Shilingi milioni moja,” amesema.
Kiongozi huyo amemwambia Rais kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza maono na wametumia maonyesho ya wakulima Nane Nane kutoa elimu ya fedha ambako wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa.
No comments:
Post a Comment