Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 12 August 2024

HUDUMA YA KIBENKI KWA WANAFAMILIA NI MOJA YA NGUZO ZA BENKI YA STANBIC

Meneja Mkufunzi wa Benki ya Stanbic Tanzania upande wa wateja Maalum, Irene Bizere, akitoa mafunzo ya kuweka akiba kwa baadhi ya watoto wa wateja maalum wa benki hiyo. Mafunzo hayo yalifanyika jijini Dar ers Salaam.
Mshauri Mwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Richi Ndisi akitoa mafunzo ya matumizi ya fedha kwa baadhi ya watoto wa wateja Maalum wa benki hiyo.
  • Inalenga kukuza stadi za awali za kifedha kwa wanafamilia.
  • Huduma inayowezesha watoto kupata uelewa wa masuala ya kifedha.
  • Stadi hizi za awali hutolewa kwa njia ya elimu kwa vitendo.
Dar es Salaam, Agosti 2024: Idara ya wateja maalumu ya Benki ya Stanbic Tanzania inajivunia kuwa na huduma ya stadi za awali ya elimu ya kifedha kwa wanafamilia hasa watoto na vijana. Tukio hilo lilifanyika jumamosi iliyopita katika Tawi lao la Peninsula huko Masaki.

Huduma hiyo imeanzishwa ili kuwapatia watoto ujuzi wa kifedha, ikiwemo njia mbalimbali za kutafuta fedha, matumizi sahihi ya fedha, utunzaji na akiba binafsi. Kwa kuwapatia watoto elimu ya kifedha, Benki ya Stanbic Tanzania inatarajia kuwajengea nidhamu na uelewa wa kifedha unaohitajika katika utunzaji wa fedha kwa ujumla .

"Tunaamini kwamba ujuzi wa kifedha ni ujuzi muhimu wa maisha ambao unapaswa kukuzwa tangu umri mdogo," alisema Irene Bizere, Meneja wa Wateja Maalumu wa Benki ya Stanbic Tanzania. "Kupitia mpango huu, tulilenga kuwezesha kizazi kijacho kwa maarifa na zana wanazohitaji kwa kufanya maamuzi sahihi ya kifedha."

Tukio hili lilikuwa na aina mbalimbali za mafunzo shirikishi yaliyoimarisha dhana za kifedha ambazo watoto walikuwa wameelimishwa. Mojawapo ya stadi walizofundishwa vijana hao ilikuwa kupanga bajeti. Mafunzo yaliendeshwa kwa njia ya vitendo kupitia uigizaji ya namna bora ya utunzaji wa fedha.

Mafunzo kama haya yana faidi nyingi ambazo watoto watakuwa nazo hadi umri wa mtu mzima. Zaidi ya hayo, watoto walio na ujuzi wa kifedha wana uwezekano mkubwa wa kuepuka madeni yasiyo ya lazima, kujiokoa kwenye matukio muhimu ya maisha, na hivyo kuchangia vyema katika uchumi wa nchi yetu na kuwapatia suluhisho mbalimbali.

"Mpango huu unasisitiza dhamira yetu na sio kuwapatia suluhisho za kifedha wateja lakini pia kuwapa wapendwa wao na wanafamilia wao huduma kama hii," aliongeza Irene."

No comments:

Post a Comment