Zaidi ya wasichana 2000 wenye umri kati ya miaka 14-18 kutoka shule za sekondari zilizopo kutoka mikoa ya Mwanza,Mbeya Arusha,Dodoma na Dar-es-saalam wanatarajia kunufaika na mradi wa ‘Code Like a girl’ wenye lengo la kuhamasisha masomo ya Sayansi, Hisabati na Teknolojia(STEM).
Akizungumza wakati wa ufundishaji wa masomo hayo jana katika chuo cha Ualimu Butima,Mratibu wa mradi huo kutoka Tanzania Data Lab(DLab),Somoe Mkwachu amesema mradi huo wanashirikiana na kampuni ya Vodacom.
"Katika mradi wetu tunafundisha wanafunzi kutumia Kompyuta katika masomo yao pia. Huwa tunachagua wanafunzi kuanzia 70 kutoka shule pendekezwa na kuwapa elimu ya kompyuta kwa muda wa siku tano haswa wakati wanapokuwa Likizo" amesema.
Amesema programu hiyo huwa inafanyika katika kipindi cha likizo za shule kama vile mwezi wa sita, likizo fupi ya mwezi wa 9 pamoja na mwezi wa 12.
Amepongeza juhudi za wanafunzi hao wanapokuwa wanafundishwa masomo hayo wamekuwa wakionyesha bidii kubwa sana ya kutaka kujua masomo.
Naye Meneja mwandamizi wa Vodacom, Kanda ya Ziwa Victoria Chale amesema lengo la kampuni yao kuhamasisha watoto wa kike teknolojia ili waweze kujua hata wao wanaweza masomo ya Sayansi.
No comments:
Post a Comment