Juni 14, 2024, Dar es Salaam – Sahara Ventures yatangaza rasami tukio la Sahara Sparks 2024 litakalo fanyika tarehe 27 na 28 Septemba katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Tanzania. Sahara Sparks ni jukwaa linalo waleta pamoja wabunifu mbalimbali wa teknolojia, wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo na teknolojia na kuwapa fursa ya kushiriki maonesho ya kibiashara pamoja na kujadili maswala mbalimbali ya teknolojia, maendeleo na uchumi.
“Wiki ya Sahara Sparks imeandaliwa kwaa ajili yetu kwahiyo wote tushiriki hususani kampuni changa za ubunifu wa teknolojia zinazo fahamika kama Startups, sekta binafsi na wadau mbalimbali tutumie fursa hii kama njia ya kutangaza biashara zetu kwa kupitia maonesho yatakayo fanyika mlimani city mwezi Septemba mwaka huu, pia tushiriki mijadala ili kwa pamoja tutatue changamoto za ujuzi na ajira” alisema Mhandisi Mwela
Mkurugenzi mtendaji wa Sahara Ventures Bw. Jumanne Mtambalike sambamba nakuhamasisha ushiriki wa wadau mbalimbali alielezea umuhimu wa mijadala itakayo fanyika katika wiki ya Sahara Sparks 2024.
“Mwaka huu tutaandaa mijadala mbalimbali itakayo anagazia namna gani teknolojia, ubunifu na ujasiliamali unavyosaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa. Majadiliano haya yatatilia mkazo zaidi kuhusu rasilimali watu hususani vijana na jinsi ya kuwaandaa kwaajili ya ulimwengu mpya wa ajira.” alisisitiza Bw. Mtambalike.
Sahara Ventures inakaribisha sekta binafsi, startups, washirika wa maendeleo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watunga sera, wataalamu wa uvumbuzi na teknolojia, wajasiriamali na wadau wengine kushiriki tukio hili la kihistoria. Kwa taarifa zaidi ya jinsi ya kushiriki au kudhamini tembelea tovuti ya www.saharasparks.com
No comments:
Post a Comment