Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Foreign Exchange Rates
CRDB Bank Advert_070325
Selcom Pesa Advert_110225
Standard Chartered Advert_300125
DStv Advert_090724
Wednesday, 12 June 2024
BENKI YA NMB YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 57.4 KWA SERIKALI
Benki ya NMB imetoa gawio la Shilingi Bilioni 57.4 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kiashiria cha azma ya kuleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wao wote, ikiwemo Serikali yenye umiliki wa 31.8% katika Benki yetu.
Kwa mwaka huu, hili ni Gawio kubwa zaidi kutolewa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka taasisi za kibiashara ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea mfano wa hundi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NMB - Dkt. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Bi. Ruth Zaipuna katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna alisema: “Kutokana na mazingira wezeshi na uimara wa sekta ya kibenki, NMB ni miongoni mwa mabenki yaliyokua sana. Gawio la jumla limeongezeka kutoka Shilingi bilioni 97 mwaka 2021, hadi kufikia bilioni 181 mwaka 2023. Gawio kwa Serikali limeongezeka kutoka Shilingi bilioni 30.8 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 57.4 mwaka 2023.”
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia ameipongeza Benki ya NMB kwa matokeo mazuri ya kiutendaji yaliyopelekea kuongezeka kwa faida kwa taasisi na gawio kwa Serikali.
Wakati wa hafla hiyo, Rais Samia pia aliikabidhi tuzo Benki ya NMB kutambua mchango wao katika kutoa gawio kubwa kwa Serikali mwaka hadi mwaka.
“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya,” alimalizia Bi. Zaipuna.
No comments:
Post a Comment