Dar es Salaam: Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum inayolenga kuwashawishi wateja wake wanaomiliki simu za mkononi kufanya miamala zaidi kwa kutumia simu zao pamoja na kutumia mtandao badala ya malipo ya fedha taslimu pindi wanapohitaji kutumia huduma mbalimbali za kibenki. Kampeni hii ya miezi mitatu itaambatana na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kila wiki na mwezi kwa washindi.
“Kila wiki, kutakuwa na droo na wateja 10 watakaobahatika watapata nafasi ya kujishindia zawadi ya fedha taslimu TZS. 50,000/=.’’ Alitaja, huku akiongeza: “Aidha, kila mwezi kutakuwa na droo ambapo wateja 10 watapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu TZS 100,000 huku sifa ya chini katika droo hii ya mwezi ikiwa ni mhusika kufanya miamala yenye thamani ya TZS 200,000 na zaidi katika huduma moja au zaidi.''
Huduma za kibenki za simu na mtandaoni za Exim Bank zimeundwa kurahisisha maisha ya mteja kwa kuhakikisha upatikanaji, urahisi, na usalama wa miamala yake. "Tunataka wateja wetu wafurahie urahisi na manufaa ya huduma za kidigitali huku wakiwa salama na kufurahia ufanisi wa miamala yao," alisema Lyimo.
Silas Matoi, Mkuu wa Njia Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali, alisema, "Ubunifu wa kidijitali ni msingi wa mkakati wetu. Kampeni ya Tap Tap Utoboe imeundwa kuhusisha watumiaji wa teknolojia na wale wasioijua sana, kuhakikisha kila mmoja anafaidika na huduma zetu."
Akizungumzia zawadi kuu kwa washindi wa kampeni hiyo, Silas alisema “Hivyo basi mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya gari mpya kabisa aina ya Mazda CX-5 ambayo iko tayari kuingia barabarani, iliyokatiwa bima kubwa (comprehensive). Mshindi wa pili yeye ataondoka na Bajaj na mshindi wa tatu atajipatia pikipiki”.
“Tunajivunia ushirikiano wetu na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania katika kampeni hii. Ushirikiano huu ni endelevu na unalenga kuhakikisha kampeni hii inafanyika kwa ubora na ufanisi mkubwa” aliongeza.
Kupitia kampeni hii ya 'Tap Tap Utoboe', Exim Bank inalenga kukuza uchumi jumuishi kwa kuwapa wateja fursa sawa za kupata huduma za kifedha. Huduma za kibenki za simu na mtandaoni za Exim Bank zinatoa fursa kwa watu wote, wakiwemo wale wa vijijini, kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi. Hii inasaidia kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema dhamira ya msingi ya benki hiyo ni kuandaa jamii yenye utamaduni wa kutotembea na pesa taslimu na badala yake wafanye miamala kwa njia za kielectroniki hatua ambayo pia imekuwa ikipigiwa chapuo na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia katika kufanya miamala ya kifedha.
“Benki yetu kihistoria imekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi ya kihuduma hapa nchini. Katika kufanikisha mageuzi hayo tumekuwa tukitumia namna mbambali ikiwemo kutoa zawadi kwa wateja wetu ili tu tuweze kwenda nao sambamba katika mageuzi haya. Tunaamini kupitia kampeni hii tunakwenda kuleta mabadiliko yenye tija na faida kubwa kwenye mfumo mzima wa sekta ya fedha hapa nchini na iatawapa wateja wetu fursa ya kufurahia huduma za kibenki zenye urahisi wa matumizi, upatikanaji wa haraka, na uaminifu. Hii ni sehemu ya kujitolea kwetu katika kuboresha huduma kwa wateja wetu na kuwahamasisha kutumia huduma zetu za kidijitali’’ alisema.
No comments:
Post a Comment